1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mali baada ya uchaguzi

14 Agosti 2013

Walimwengu wasifu jinsi uchaguzi ulivyopita nchini Mali na kushusha pumzi baada ya Ibrahim Boubacar Keita kuibuka na ushindi

https://p.dw.com/p/19Orp
Mkuu wa matangazo ya DW kwaajili ya bara la Afrika Claus StäckerPicha: DW

Uchaguzi wa Mali umepita vizuri. Ulikuwa uchaguzi wa kuaminika na uliofanyika kwa njia ya uwazi kama walivyosema wasimamizi wa Umoja wa ulaya. Na mshindi pia ni mtu anaefaa.Hivyo ndivyo wasemavyo angalao wadadisi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya kuhusu kuchaguliwa Ibrahim Boubakar Keita.Kiongozi mpya ambae kila mtu anamwita IBK, kwanza kabisa ni mtu wa Ufaransa. Rais Francois Hollande hajasubiri matokeo rasmi yatangazwe ili kumpongeza.

Ni ushindi kwaajili ya demokrasia na Ufaransa itashirikiana nae-ameahidi rais Hollande. Keita amesomea na kuhitimu masomo yake nchini Ufaransa. Aliongoza mradi wa Umoja wa ulaya na kufanyakazi pamoja na shirika linalopigania haki za binaadam la Terre des Hommes. Kampeni yake ya uchaguzi ilisimamiwa na shirika moja la Ufaransa. Anatajikana kuwa mtu wa kutegemewa na muaminifu. Viongozi wa mjini Paris kwa hivyo wameridhika.

Lakini hata viongozi wa Berlin wamepumuwa.Keita ni mtu wa Ujerumani pia.Serikali kuu ya Ujerumani inamjua vizuri,hata kama imeonya:mtangulizi wake,Amadou Toumani Touré pia alikuwa akisifiwa hadi alipopinduliwa mwaka 2012.Mali na Ujerumani zina uhusiano mzuri na wa jadi.Mjini Timbuktu kuna kumbusho lililopewa jina la mtafiti wa masuala ya Afrika,Heinrich Barth.Serikali kuu ya Ujerumani ilikuwa ya mwanzo kuitambua Mali ilipopata uhuru mwaka 1960. Hali hiyo inaendelea mpaka leo. Wanajeshji wa Ujerumani wanapatiwa mafunzo katika ardhi ya Ujerumani.Kuna ushirikiano wa kirafiki kati ya miji ya Ujerumani na Mali. Vuguvugu la demokrasia lilipoanza Mali mapema miaka ya 90,wanasiasa kadhaa wa Ujerumani waaliitembelea nchi hiyo, kuanzia rais wa shirikisho,waziri wa mambo ya nchi za nje, yule wa misaada ya maendeleo,waziri wa ulinzi na spika wa bunge pia. Biashara kati ya Mali na Ujerumani ilifikia katika mwaka 2010 Euro milioni 70.

ABK awekewa matumaini ya kuipatia ufumbuzi mizozo nchini Mali

Mali ilikuwa ikiangaliwa kama mfano wa kuigizwa,vuguvugu la demokrasia lilipopiga barani Afrika.Na katika eneo la Sahel Mali ilikuwa ikiangaliwa kama kisiwa cha matumaini mema na utulivu hadi mapinduzi yalipotokea.Rais mpya hajawahi hata mara moja kulaani mapinduzi hayo na hajaficha pia aliposema katika mahojiano na shirika la habari la ujerumani DPA tunanukuu:"utakuaje rais kama huna imani na jeshi?

Kwamba Keita ni mtu wa wanajeshi, hakuna ubaya. Hata hivyo amefanikiwa pia kupata uungaji mkono wa wachamngu wa kiislam. Hafichi, hotuba zake zote anazianza kwa kujitaja kuwa yeye ni muislam. Yeye pia ni mtoto wa umma,amechaguliwa kwa njia za haki na bayana. Shaka shaka ziligubika uchaguzi huo,lakini maajabu ni kwamba wamali wengi zaidi wameteremka kutoa sauti zao kuliko wakati wowote ule mwengine na tena licha ya mvua kali, matope na shida nyenginezo.

Na wamempa sauti zao mtu anaejulikana aliyewahi muda mrefu kuwa kiongozi wa chama cha rais wa zamani ,aliyepanda daraja hadi kufikia cheo cha waziri mkuu. Wakati ule alijipatia sifa ya "Kankeletegui" ikimaanisha kwa lugha ya Bambara" mtu mwenye kutekeleza alichoahidi." Pengine wanampa cheo cha baba,mwenye uwezo wa kuleta suluhu ambayo Mali inaihitaji kupita kiasi.

Mwandishi: Stäcker,Claus/Hamidou Oummilkheir.

Mhariri: Mohammed Khelef