1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Steinmeier rais wa kinyume na matarajio

Mohammed Khelef
14 Novemba 2016

Muungano wa CDU/CSU umetangaza kumuunga mkono Waziri wa Mambo ya Nje, Frank-Walter Steinmeier, kuchukuwa nafasi ya Rais Joachim Gauck, ukimfungulia njia kupita kirahisi kwenye nafasi hiyo yenye heshima kubwa kisiasa.

https://p.dw.com/p/2Sfsf
Deutschland Steinmeier wird neuer Bundespräsident
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Gambarini

Lilikuwa onyesho la aina yake kwenye ofisi ya juu kabisa ya kisiasa na sasa ni miezi mitano sasa tangu Rais Joachim Gauck wa Shirikisho la Ujerumani kutangaza kutowania tena kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo hapo mwakani na, hivyo, kusababisha tafrani kwenye kichwa cha Kansela Angela Merkel, ambaye pia ndiye kiongozi wa chama cha CDU. 


Baada ya kuwapoteza Horst Köhler na Christian Wulff mwaka 2004 na 2010, kuja madarakani kwa Gauck kulionekana kulazimishwa kwake na chama cha kiliberali cha FDP, ambacho kilikuwa mshirika mdogo kwenye serikali ya mseto mwaka 2012. 

Safari hii, akiwa anasitasita na kugomagoma, kwa mara nyengine Kansela Merkel akajikuta analivaa suala hili na kisha kwa ghafla akajikuta anaondokana na khofu zake alizokuwa nazo. Ingawa muungano anaouongoza wa CDU na CSU ndio wenye nguvu kubwa kwenye Bunge la Shirikisho, na kwamba muungano huo ungelikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumtoa mgombea wao wa nafasi ya uraisi, hakuna ndani ya kambi hii ya kihafidhina aliyekuwa  na hamu na kazi hiyo. Siku, wiki na hata miezi imekatika, huku Kansela Merkel akisaka mtu, lakini hatimaye ameangukia patupu. 

Kosa moja, goli moja

Lakini kwa mkuu wa chama cha SPD, Sigmar Gabriel, hii ilikuwa ni fursa aliyokuwa akiisaka ya kufanya mapinduzi ya kisiasa. Pasina kutoa ishara yoyote, akamleta kamanda wa chama chake, Frank-Walter Steinmeier, mchezoni. Fursa ya kipekee, goli la kipekee.
Laiti kungelikuwa na maelekezo ya kazi ya rais wa shirikisho, basi waziri huyu wa sasa wa mambo ya nje ndiye pekee anayeweza kujaa kwenye kiti hicho: akili, mtu wa mchanganyiko, mwanadiplomasia, mwenye kualakiana na watu.

Ingawa Steinmeier si mzungumzaji sana, lakini aina yake ya kuzungumza inamuweka kwenye nafasi kubwa zaidi kuliko ya kidiplomasia. Mwezi Agosti alimpa somo Donald Trump juu ya hotuba zake za chuki na hata rais huyo mteule wa Marekani alipochaguliwa mwezi huu, amekataa hadi sasa kumpongeza.

Hata Kansela Merkel anampenda Steinmeier. Kibinaadamu wanaonekana kuendana kisiasa kwa kuwa wana maono ya pamoja. Lakini kinachomuweka njia panda Kansela Merkel ni kuwa Steinmeier ni mwanasiasa aliye kwenye chama kisicho sahihi kwake. Kama mtu anauangazia uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, basi ni jambo lisiloingia maanani kwa Kansela Merkel kumchagua mgombea wa SPD. 

Ndio maana alijitahidi kadiri awezavyo kuzuia maridhiano ya kumuidhinisha Steinmeier kuwa mgombea kutoka kwa CDU, CSU na hata akatafautiana wazi wazi na Waziri Mkuu wa mkoa wa Baden-Wuttenburg kupitia chama cha Walinda Mazingira, Winfried Kretschmann. Lakini, hatimaye, ndiyo vyama vikuu vimeshampitisha Steinmeier na hili ni pigo la wazi kwa Kansela Merkel.

Mwandishi: Sabine Kinkartz
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Saumu Yussuf
 

Kinkartz Sabine Kommentarbild App
Na Sabine Kinkartz