1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Tarehe 9 Novemba 1989 - Siku isiyosahaulika

9 Novemba 2014

Ujerumani inaadhimisha robo karne ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, tukio ambalo lilitokana na mapinduzi ya umma yaliyofanywa kwa njia za amani na kupelekea kuungana tena kwa taifa lililogawika.

https://p.dw.com/p/1DjXs
25 Jahre Mauerfall - Lichtergrenze
Taa zilizopangwa umbali wa kilometa 15 mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa/J. Kalaene

Siku ya karne, siku ya Wajerumani - hayo na mengine mengi yalikuwa tarehe 9 Novemba 1989. Hususan kwa wananchi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki (GDR), lakini pia hata Jamhuri ya Ujerumani, na pia kwa bara la Ulaya.

Novemba 9, 1989, ilikuwa ni wakati usioelezeka. Kutoka wakati uongozi ulipotoa matamshi yakutatanisha jioni moja kabla, kwamba kila mtu ataruhusiwa kusafiri atakako, hadi kuanguka kwa ukuta jioni ya tarehe 9 na hadi usiku. Katika muda wa masaa machache maisha ya Wajerumani na watu wa Ulaya yalibadilika.

Historia imetokea. Ujerumani mashariki , eneo lililokuwa likitawaliwa na wakomunisti, limeanguka kutokana na mbinyo wa waandamanaji na wale waliokuwa wakikimbia. Kuanguka kwa ukuta ilikuwa mwisho wa utawala wa Ujerumani mashariki, licha ya kuwa muungano wa Ujerumani mbili ulitokea mwaka mmoja baadaye.

Ujerumani mashariki bila ukuta na uzio wa waya, kuwaruhusu raia wake wasafiri watakako ,hakuna maana, wananchi ambao hawana haki ya kuishi tena - isipokuwa katika maeneo ya kambi ya mashariki na nchi za mkataba wa Warsaw pekee.

Gorbatschov mwanamapinduzi

Lakini iliyokuwa Umoja wa Kisoviet , ukiongozwa na mwanamapinduzi Gorbatschov , ilijitenga na matumizi ya nguvu, kama ilivyokuwa pia kwa uongozi wa Berlin mashariki, katika kile kinachojulikana kama " suluhisho la Uchina", kama mauaji yaliyotokea katika uwanja wa amani mjini Peking, hayo hayakutokea.

DW 60 Jahre Alexander Kudascheff
Alexander KudascheffPicha: DW/Matthias Müller

Tarehe 9 Novemba mwaka 1989 vuguvugu la kudai kuwa huru halikukandamizwa kinyama kama ilivyotokea mwaka 1953 katika Ujerumani mashariki, mwaka 1956 nchini Hungary,na mwaka 1968 katika Czech Slovakia . Kuanguka kwa ukuta kumekamilisha mapinduzi ya amani katika Ujerumani mashariki.

Tarehe 9 Novemba ilikuwa usiku wa furaha kubwa na machozi ya furaha. Siku hii imekuwa ya hisia kubwa kwa Wajerumani. Ni siku ya watu ambao walisahaulika na siku ya hisia kali, ikiwa ni siku watu waliokuwa wakiitarajia ya muungano kwa pande zote, siku kila mmoja alikuwa akiitamani kwa ajili ya uhuru katika upande wa mashariki.

Ilikuwa kama hali ya ulevi, ambapo Wajerumani na wakaazi wa mji wa Berlin iliwaelemea. Hisia za furaha , ambazo wakati ule "zilituacha tumeshangaa". Siku moja , usiku mmoja , hisia zisizoelezeka , kwamba mtengano wa miaka 40 haukuweza kuvunja hisia za udugu, hali hii baadhi yetu pia imetushangaza.

Ukuaji wa pamoja

Na maneno haya mazuri ya Willy Brandt, "sasa kitamea kwa pamoja kile ambacho kilikuwa pamoja". Lakini ni ukuaji wa pamoja , ambao hakuna mtu aliyeweza kuufikiria , hususan sio dhidi ya jirani. Mapinduzi ya amani yameiweka Ujerumani katikati ya Ulaya.

Vuguvugu la maandamano Ujerumani mashariki limepambana na udikteta wa kikomunist, dhidi ya wale wote waliokuwa wakitawala kwa mabavu. Yalikuwa ni mapambano ya kutaka taifa huru na la uwazi, ambamo mtu hatawekewa tena vizuwizi.

Ndio sababu inachekesha kuona kwamba , vinasaba vya kisiasa vya Ujerumani iliyoungana vinakubaliana na matamanio ya Wajerumani upande wa magharibi na Mashariki baada ya mahitaji hayo makubwa ya taifa. Uasi dhidi ya taifa ulikuwa uasi dhidi ya wale waliokuwa juu, lakini sio uasi kwa jamii ya uwazi.

Ujerumani baada ya tarehe 9 Novemba imekuwa hatua kwa hatua pamoja, na kuondokana na hali ya umashariki na nadharia zake, migongano michache ya kinadharia, na mtu anaweza kusema pia , imeelekea zaidi mrengo wa shoto. Na inauwakilishi na kutawaliwa na Wajerumani wawili kutoka Ujerumani mashariki, rais wa shirikisho la Ujerumani Joachim Gauck na kansela Angela Merkel.

Wote hawa mtu anaweza kutambua uzoefu wao ndani ya iliyokuwa Ujerumani mashariki. Na kwa upande wa fursa hilo linaweza pia kujadiliwa. Lakini pamoja na hayo ni hali ya kawaida ya kisiasa , mashariki na magharibi haziwezi tena kutengana.

Umoja uliopo ni mpana zaidi kuliko wengi wanavyofikiria. Na watu wameanza kupata hisia za furaha za Novemba 9 , 1989.

Mwandishi: Alexander Kudascheff

Tafsiri: Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef