1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Ujerumani yapata serikali mpya

17 Desemba 2013

Ujerumani hatimaye imepata serikali mpya mwishoni mwa juma. Mzigo mkubwa wa kazi unaoikabili serikali ya mseto hata hivyo unahitaji wakati kama inavyoelezwa katika maoni ya mwandishi wa DW Henrik Boehme.

https://p.dw.com/p/1AaBQ
Henrik Boehme
Henrik BoehmePicha: DW

Uchumi wa Ujerumani ndio pekee ambao unaonekana kuwa haukupata misukosuko mikubwa katika mzozo wa kifedha barani Ulaya.

Mauzo ya nje yanakwenda vizuri, soko la kazi linaonekana kuwa imara na mapato ya kodi ni makubwa. Mafanikio haya yamekuja kwa njia nyingi,

Mafanikio yanatokana na sababu nyingi, mojawapo ikiwa ni wafanyabiashara werevu pamoja na vyama vya wafanyakazi kuwa na uwezo wa kufanya makubaliano, na pia uchaguzi uliofanyika mwezi Septemba ambapo vyama vya kihafidhina vilivyokuwa vinaunda serikali vimerejeshwa madarakani licha ya chama cha FDP kutupwa nje.

Ukiangalia mkataba wa serikali ya mseto, ambamo vyama vya CDU, CSU na SPD vimeweka malengo yao kwa muda wa miaka minne ijayo pamoja na msingi wa utendaji wa serikali hiyo, mtu anaweza kuwa na shaka , kwamba historia ya mafanikio ambayo Ujerumani imefanikisha katika miaka ya hivi karibuni haitaweza kuendelezwa.

Mkwamo badala ya mwanzo mpya

Kile ambacho vyama vya CDU na SPD vimeweka kama msingi wa utendaji wao,kinaonekana kuwa kinaweza kuzusha mkwamo badala ya mwanzo mpya. Hakuna ishara kamili, kuwa Ujerumani itakuwa kiongozi katika maendeleo ya teknolojia na kupambana na ushindani mkubwa kutoka bara la Asia. Kwa kweli inaonekana kuwa ni hali ya bora liende tu.

Maneno ya msingi manne yanatosha: Mabadiliko ya kieneo, miundo mbinu, elimu, mabadiliko katika nishati. Pekee mabadiliko hayo ya mwelekeo katika masuala ya nishati ni suala zuri sana, ambapo hadi sasa ilikuwa hakuna mwelekeo sahihi.

Hivi sasa kutakuwa na "waziri kamambe", ambaye ni mwenyekiti wa chama cha SPD Sigmar Gabriel, atakayechukua wajibu wa nafasi ya waziri wa uchumi na pia nishati.

Nishati endelevu

Kitu gani kitakuwa kizuri zaidi katika hilo, bado haiko wazi.

Wizara ya uchumi ambayo inategemea viwanda inakuwa ni njia ya ubadilishaji mwelekeo wa makampuni makubwa ya nishati? Pia katika wiki zijazo kutakuwa na mtafaruku, iwapo halmashauri ya Umoja wa Ulaya itaidhinisha, hatua dhidi ya Ujerumani , kwa sababu mahitaji ya vyanzo vya umeme usioharibu mazingira kutokana na changamoto mbali mbali unahitajika. Hapo kutakuwa na vikwazo vingi dhidi ya wizara.

Kwa kweli naweza kuyaweka matatizo hayo pamoja na matatizo mengine. Kwa upande wa miundo mbinu Ujerumani imo katika matatizo. Kwa sababu serikali mpya imeamua dhidi ya kutoza ushuru wa barabara kwa kuwa fedha zinazotarajiwa hazitatosha kujenga barabara, njia za reli na mifumo ya digitali kwa ajili ya hapo baadaye.

Sitajaribu kutabiri , kwamba muungano huu mkuu hautaweza kuleta mafanikio. Hiyo itakuwa ni hali mbaya ya kutoiamini, na hususan chama cha SPD ambacho mipango yake mingi imepangwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2017.Wakati huo bunge jipya litakuwa limechaguliwa. Hali lazima itakuwa tofauti kabisa, iwapo hali mwishowe haitakuwa nzuri. Itakuwa ni miaka minne iliyopotea bure kwa Ujerumani.

Mwandishi : Böhme , Henrik / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Hodali Diana/Daniel Gakuba