1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni : Uvumi wa vitisho haufanyi kazi tena

4 Oktoba 2016

Kura ya maoni ilioshindwa inaonyesha kiburi cha majigambo ya Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban kimeanza kufifia Hungary jambo ambalo mwandishi wa DW Max Hoffmann anasema linapaswa kuufurahisha Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/2QqxP
Ungarn Orban gibt Statement zum Referendum ab
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban.Picha: Reuters/L. Balogh

Iwapo ulikuwa ukisikiliza kwa makini Jumapili jioni yumkini ukawa umesikia kicheko cha inda kutoka kwa jengo la Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels.Kiuhalisia hata kura ya maoni ambayo ingelikuwa inafaa isingeliweza kusababisha mabadiliko makubwa kwa sera ya wakimbizi ya Umoja wa Ulaya angalau Orban amechapwa na watu wake mwenyewe na sio tu viongozi wa taasisi za Umoja wa Ulaya.Uzushi wa vitisho wa Orban hauwezi tena kuvutia idadi kubwa ya wapiga kura vituoni hata nchini Hungary kwenyewe.

Lengo lilikuwa wazi wananchi wa Hungary walikuwa watamke tena kwa kila mtu barani Ulaya kwamba hawataki kuwaingiza nchini mwao wakimbizi wowote wale katika nchi hiyo yenye wakimbizi 2,300 tu.Fikra ilikuwa ni kwa kila mtu barani Ulaya kuupata ujumbe huo : Mawaziri wote walisema hilo,Orban amelisema hilo na hivi sasa wananchi pia wamesema.

Tatizo ni kwamba wengi wao walikuwa hawataki kulisema hilo.Kati ya asilimia 45 waliopiga kura ni kweli kwamba wengi walikuwa upande wa Orban. Hata hivyo kura hiyo ya maoni ilitambulika kama ni batili na hii sio alama ya ushindi ambayo serikali ya Hungary ilikuwa ikitaka kuituma.

Deutsche Welle Studio Brüssel Max Hofmann
Max Hofmann mwandishi wa DW.Picha: DW/B. Riegert

Kwa hiyo kura hiyo ya maoni inatueleza nini ?

Batili au hapana, inayakinisha tu kile tulichokuwa tukikijuwa kwa muda mrefu kupitia uchunguzi wa maoni : Wananchi wengi wa Hungary walikuwa hawataki kuwaingiza wakimbizi nchini humo. Pia imeonyesha kwa mara nyengine tena kwamba Viktor Orban amejiandaa kuendelea kuwaudhi washirika wake katika Umoja wa Ulaya kwa kadri makakati huo utakapokuwa unaendelea kufanya kazi kwa faida yake nchini mwake.

Hata hivyo jambo hilo hivi sasa linaonekana kuanza kufikia ukingoni taratibu.Kura hiyo ya maoni iligharimu euro milioni 40.Orban alibandika mabango nchini kote Hungary akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura lakini wachache waliitikia wito huo na kuashiria kwamba baadhi ya wananchi wake wamechoshwa na kiburi cha majigambo ya Orban.

Ili sera zake mchanganyiko za kucheza na hisia za watu ziendelee kufanya kazi inabidi aendelee kuzusha hofu ya kuanguka kwa ustaarabu wa mataifa ya magharibi.Kwa maneno mengine inabidi aongeze kiwango cha dawa au dozi kama ilivyofanya kwa kura hiyo ya maoni ili kupata matokeo yanayotakiwa.

Tokea kura ya maoni ya kujitowa Uingereza Umoja wa Ulaya Brexit imekuja kuwa wazi kwamba kukubaliana kwa kiasi fulani wakati wa Mikutano ya kilele ya Umoja Ulaya halafu kuitisha kura ya maoni nyumbani dhidi ya maamuzi ya Umoja wa Ulaya yanayotakiwa kutekelezwa kisheria bila ya shaka sio njia muafaka ya utendaji .Wakati umefika kwa Viktor Orban kulifahamu hili.Kushindwa kwa kura hiyo ya maoni kumeleta matumaini kwa raia wengi wa Huangary kwamba utambuzi huo tayari umebainika kwa manufaa ya Umoja wa Ulaya.

Mwandishi : Max Hoffmann/Mohamed Dahman

Mhariri: Gakuba Daniel