1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Vyombo vya habari

Maoni: Vyombo vya habari viheshimu wenye mawazo tofauti

Oumilkheir Hamidou
3 Mei 2017

Hata katika nchi za kidemokrasia, waandishi habari wanazidi kutiwa vishindo katika shughuli zao. Vyombo vya habari vinachangia katika hali hiyo, anasema mhariri mkuu wa DW Ines Pohl katika uhariri wake.

https://p.dw.com/p/2cGio
Maandamano ya kudia uhuru wa vyombo vya habari
Picha: picture-alliance/dpa/S. Suna

Takwimu zinatisha: Idadi ya waandishi habari, wake kwa waume wanaotiwa vishindo , wanaozuwiliwa kufanya kazi yao, na wakati mwengine kufika hadi ya kukabiliwa na vitisho, kufungwa au kuuliwa inazidi kuongezeka ulimwenguni. Licha ya juhudi zote za kimataifa, serikali katika nchi mfano wa Misri au Burundi zinawaandama waandishi habari bila ya kujali chochote.

Nchini Uturuki, hali ya waandishi habari na vyombo vya habari imeharibika vibaya sana kufuatia wimbi la ukandamizaji lisilokuwa na mfano tangu njama iliyoshindwa ya mapinduzi msimu wa kiangazi mwaka jana. Zaidi ya waandishi habari 150 wametiwa ndani miongoni mwao ni mjerumani mwenye asili ya Uturuki Deniz Yücel. Katika nchi zinazogubikwa na vita na mizozo mfano wa Syria, Afghanistan, Iraq au Yemen waandishi habari wanakabiliwa mtindo mmoja na hatari ya kupoteza maisha yao. Ndio maana kazi ya vyombo vya lugha tofauti vya  habari vya kimataifa ni muhimu kupita kiasi - majukumu yao hayatuwami pekee katika kufikisha habari za kuaminika katika yale masoko ambayo habari za kuaminika ni marufuku.

Vitisho kwa wanahabari

Ines Pohl, mhariri mkuu wa DW
Ines Pohl, mhariri mkuu wa DWPicha: DW/P. Böll

Zaidi ya hayo kuna tukio jengine la kutisha. Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la "Maripota wasiokuwa na Mipaka" inadhihirisha kwamba hata katika zile nchi ambako m fumo wa kidemokrasi umekomaa, uhuru wa vyombo vya habari unabanwa kwa nguvu kupita kiasi. Matamshi ya chuki dhidi ya vyombo vya habari yanaonyesha kuwavutia sana wanasaiasa wa nchi mfanao wa Marekani au Poland, hali inayowafungulia njia ya kuweka sheria kali, kuimarisha madaraka ya idara za upelelezi na kuwatisha wale wote wanaofichua mambo.

Na hasa Donald Trump aliyefanikiwa katika kampeni zake za uchaguzi kwa kipindi cha miezi michache tu kushuku ubora wa ripoti za avyombo mashuhuri vya habari.Yeye ndie anaetumia mtandao wa Twitter kila siku kueneza habari zisizokuwa na uhakika wowote na kuwafikia mamilioni ya watu.Mara nyingi anaeneza habari za uwongo na mara chungu nzima pia anazitaja habari za kuaminika kuwa ni habari za uwongo. Na hasa kama habari hizo zinamkosoa au zinakosoa sera zake.

Kwa kufanya hivyo anawakosha sio tu wafuasi wake.Mpaka wanaomkosoa vikali rais huyu mpya wa Marekani wanakubaliana na hoja kwamba vyombo vya habari si huru tena.Vina walakini na sehemu ndogo tu ya yale yanaosemwa ndiyo ambayo binaadam wa kawaida anayazingatia. Hali kama hiyo haitokei pekee Marekani, bali pia katika nchi mfano wa Poland, Ufaransa, Uholanzi na hata Ujerumani thamani ya uandishi habari wa dhati imepungua. Na kutokana na njia mpya za mawasiliano kupitia mtandao imezuka hali ambayo pengine ni kitisho kikubwa zaidi kwa uhuru wa vyombo vya habari;haali ya kupoteza imani.

Mwandishi: Ines Pohl/Hamidou Oumilkheir

Mhariri: Iddi Ssessanga