1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Wito kwa Waislamu

Admin.WagnerD5 Julai 2016

Waislamu katika nchi nyingi duniani wakijiandaa kusherehekea sikuukuu ya Eid Ul Fitri ambayo ni maadhimisho ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, nchi nyingi za ulimwengu huo zinakabiliwa na Matatizo

https://p.dw.com/p/1JJFe
Sherehe zilizopita za Eid ul Fitri katika eneo la watu masikini Pakistan
Sherehe zilizopita za Eid ul Fitri katika eneo la watu masikini PakistanPicha: DW/I. Jabeen

((Wakati Waislamu katika nchi nyingi duniani wakijiandaa kusherehekea sikuukuu ya Eid Ul Fitri ambayo ni maadhimisho ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, nchi nyingi za ulimwengu wa Kiislamu zinajikuta zikikabiliwa vile vile na ongezeko la ghasia na makundi ya misimamo mikali ya kidini sambamba na migogoro mikubwa ya kisiasa.

Waislamu takriban katika ulimwengu mzima wanajiandaa kusherehekea sikuuu ya Eid ambayo inaadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mzima wa Ramadhan.Waislamu takriban ulimwengu mzima wanajarajiwa kusherehekea sikuu ya Eid hapo kesho Jumatano ingawa wapo waislamu wachache tu walioswali Eid Hii leo ikiwemo baadhi hapa nchini Ujerumani na barani Afrika huko nchini Niger.

Mwezi mtukufu mtukufu wa Ramadhan ni mwezi ambao unamafunzo mengi ndani yake ikiwa ni pamoja na kutoa funzo la kuvumiliana,amani,kujizuia kama mtu binafsi,kuheshimu maisha pamoja na kuwajali wasiojiweza na wanaoishi katika ufukara wa kupindukia. Hata hivyo nchi nyingi za kiislamu leo hii ziko mbali sana na mafunzo hayo ya kidini na misingi yake. Kundi linalojiita dola la kiislamu siku ya Jumapili Julai 3 lililofanya mashambulizi na kuua zaidi ya watu 115 katika mji mkuu wa Iraq ni moja ya alama inayotukumbusha ni kwa jinsi gani ugaidi ni kitisho kikubwa katika jamii nyingi za kiislamu.

Shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Ataturk nchini Uturuki Juni 28,mauaji yaliyofanywa na kundi la Talibal huko Kabul Juni 30 na Tukio la utekaji nyara katika mgaghawa mmoja mjini Dhaka Bangladesh Julai 2 haya yote yanaonesha kwamba baadhi ya wanaojiita waislamu wameisaliti misingi ya imani ya kiislamu ambayo inatilia mkazo juu ya amani na kuvumiliana. Kiasi robo ya idadi ya watu ulimwenguni ni Waislamu na kwa bahati mbaya sana sehemu kubwa ya waliomasikini ulimwenguni ni jamii hiyo.Na ni jambo la kusikitisha kwamba migogoro ya kimadhehebu na kidini inashuhudiwa katika ulimwengu wa kiislamu na hasa Mashariki ya kati.

Mwandishi wa Dw-Urdu Kishwar Mustafa
Mwandishi wa Dw-Urdu Kishwar Mustafa

Ni bahati mbaya kwamba migogoro ya kisiasa,ugaidi,njaa,rushwa,mivutano ya kimadhehebu,kikabila na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ndiyo mambo ambayo kwa sasa yanayouelezea ulimwengu wa kiislamu.Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba watoto milioni 3.6 wa Iraqi wako katika hatari kubwa ya kupoteza maisha ,kuumizwa,kukabiliwa na ubakaji,kutekwa nyara na kulazimishwa kujiunga na makundi ya wapiganaji.Zaidi ya watu milioni 4.8 nchini Sudan Kusini watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo wakati ambapo kitisho cha janga la njaa kinaendelea yamesema makundi ya kutetea haki za binadamu.

Hali ya mambo katika nchi za Pakistan na Bangladesh sio tafauti,mashambulio ya kigaidi na kuongezeka kwa itikadi kali ni kadhia zinazozitikisa nchi hizo mbili za kusini mwa Asia.Lakini watawala wachache katika nchi hizo za kiislamu wanaoenekana kutoguswa kabisa wala kujishughulisha na ukweli huo wa mambo.Kwahivyo basi kwa hali kama hii kufunga Ramadhan na baadae kusherehekea Eid ni ibada zinazoonekana kuingia doa na kukosa maana halisi.Kwa maneno mengine Mfungo wa Ramadhan na sherehe za Eid ni mwito wa kumtaka kila mtu ajitathmini na kubeba dhamana.Ni matarajio ya wengi kwamba Ramadhan na sherehe za mwaka huu za Eid zitakuwa ni nafasi ya kuleta maridhiano na mjongeleano.

Mwandishi: Kishwar Mutafa DW/Saumu Mwasimba

Mhariri: Mohammed Khelef