1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya Peter Philipp.

13 Julai 2007

Mkutano mkuu wa pili juu ya kuwajumuisha raia wa kigeni katika jamii ya Ujerumani umemalizika na hisia za mgawanyiko.

https://p.dw.com/p/CHkD

Mkutano huo ulihudhuriwa na kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel,wajumbe wa jamii kadhaa za raia wa kigeni,wawakilishi wa makanisa na mashirika ya kiuchumi.

Lengo la mkutano lilikuwa kujadili mpango wa kitaifa wa kuendeleza mchakato wa kuwajumuisha raia wa kigeni katika jamii ya walio wengi hapa nchini Ujerumani

Maazimio kadhaa yamepitishwa na wajumbe juu ya kukarabati ahadi mia nne, kuanzia misaada katika sekta ya michezo na katika lugha ya kijerumani kwa ajili ya wageni .Kansea wa Ujerumani bibi Merkel amesema mkutano huo ulikuwa wa kihistoria .

Lakini katika upande mwingine mkutano huo uliibikwa na lawama kali zilizosababishwa na sheria mpya ya uhamiaji . Kwa mujibu wa sheria hiyo, ikiwa mtu anataka kuoa ama kuolewa na raia wa kigeni anaeishi Ujerumani ataruhusiwa kufanya hivyo na kuishi nchini , ikiwa atakuwa na umri wa miaka 18 ama zaidi na ikiwa atakuwa na ujuzi wa msingi wa lugha ya kijerumani.Mtu anawajibika kuwa na msamiati wa maneno angalau 300 ya kijerumani.

Kuonesha ishara ya kupinga sheria hiyo, jumuiya tatu kubwa za kituruki zilisusia mkutano wa jana na kansela Angela Merkel. Wawakilishi wa jumuiya hizo wamesema sheria hiyo ni ya kibaguzi.

Kutokana na kundi kubwa la wahamiaji kuwa waturuki, wawakilishi hao wanahisi kuwa ni waturuki wanaobaguliwa.

Lakini baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani wamepinga madai hayo. Wameeleza kuwa umri wa mhamiaji mwanamke umepandishwa kwa sababu ya kuepusha ndoa za kulazimisha na kwamba ujuzi wa msingi wa lugha ya kijerumani ni jambo la manufaa kwa watu wanaoishi nchini Ujerumani.

Lakini kipengee hicho hakitilii maanani mazingira ya Uturuki ambapo ni vigumu kujifunza lugha hiyo.Mazingira ya Uturuki ni tofauti na ya New York ama ya Tokyo.

Hatahivyo hatua ya jumuiya za kituruki imetafsiriwa kana kwamba jumuiya hizo zinataka kuishinikiza serikali ya Ujerumani.

Lakini ukweli ni kwamba kujifunza lugha ya kijerumani nchini Uturuki ni kizingiti kikubwa hata ikiwa ni maneno machache!

Na mkakati wa kuzuia ndoa za kulazimishwa hauwezi kutekelezwa kwa ukamilifu kwa kupandisha umri ,kwa wanawake wanaotaka kuja na kuolewa nchini Ujerumani.

Matatizo hayo yote yanaweza kutatuliwa nchini Ujerumani tu.

Hayo yalipaswa kuzingatiwa wakati wa kutunga sheria hiyo ya uhamiaji. Adha ingeliepushwa.

AM.