1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Afghanistan

Abdu Said Mtullya29 Novemba 2012

Wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya wanajeshi wa Ujerumani kuondoka nchini Afghanistan na juu ya maombi ya Wapalestina ya kupatiwa hadhi ya kuwa wanachama waangalizi kwenye Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/16sTB
Wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan
Wanajeshi wa Ujerumani nchini AfghanistanPicha: picture-alliance/dpa/dpaweb

Juu ya jukumu la Ujerumani nchini Afghanistan gazeti la "Märkische Allgemeine" linasema nchi za mgharibi zilijiwekea malengo mengi,baada ya utawala wa Taliban kutimuliwa nchini humo. Mhariri wa gazeti hilo anatilia maanani kwamba malengo hayo hayakufikiwa. Lakini anasema ni sahihi kabisa kwa Ujerumani na washirika wake wa magharibi kuanza kuondoka Afghanistan hatua kwa hatua.Sababu ni kwamba majeshi ya nchi za magharibi hayawezi kukaa nchini humo daima.

Mhariri wa gazeti la "Der Tagesspiegel" anasema majeshi ya nchi za magharibi yanaondoka Afghanistan kwa sababu wananchi katika nchi hizo wametumbukiwa nyongo na vita vya Afghanistan. Na gazeti la "Saschiche" linatoa ushauri kwa serikali ya Ujerumani juu ya Afghansitan kwa kusema:
Baada ya miaka 11, jukumu la kijeshi nchini Afghanistan, linakaribia mwisho kwa Ujerumani. Katika miezi 15 ijayo idadi ya wanajeshi wa Ujerumani itaendelea kupunguzwa. Lakini mpaka wakati huo jeshi la Ujerumani litahitaji helikopta za aina mpya.Mambo hayo mawaili hayatangamani. Mpaka sasa serikali ya Ujerumani haijakuwa na umaizi wa kutambua kwamba nguvu za kijeshi hazitalitatua tatizo la Afghanistan.

Gazeti la "Lübecker Nachrichten" linasema katika maoni yake kwamba sasa wakati umefika kwa watu wa Afghanistan wenyewe kulichukua jukumu la kuilinda nchi yao.Kwa hivyo ni sahihi kwa Ujerumani na washirika wake kuanza kuondoka.Mhariri wa gazeti hilo anaeleza anasema licha ya matatizo na hali zote za mashaka, watu wa Afghanistan wanapaswa kulichukua wenyewe jukumu la ulinzi. Hata hivyo haitakuwa sahihi kuwaacha watu hao peke yao ghafla.Misaada ya maendeleo na ya mafunzo itaendelea kuhitajika.

Mhariri wa "Kölner Stadt-Anzeiger" anazungumzia juu ya maombi ya Wapalestina ya kuwa wanachama waangalizi kwenye Umoja wa Mataifa kwa kuutilia maanani msimamo wa Ujerumani Anasema Israel na Marekani zinapinga vikali,Palestina kuwa nchi mwanachama mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa. Lakini nchi kadhaa za Ulaya, na hasa Ufaransa zinawaunga mkono Wapalestina. Swali kwa ,Ujerumani sasa ni moja, jee itafungamana na Israel au itashikamana na Umoja wa Ulaya?

Mwandishi:Mtullya abdu.Deutsche Zeitungen

Mhariri:Abdul-Rahman