1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya kudakizwa mawasiliano ya simu na mtandao nchini Marekani

Abdu Said Mtullya10 Juni 2013

Wahariri wanatoa maoni juu ya kashfa inayohusu kudakizwa mawasiliano ya simu na ya mitandao nchini Marekani na duniani kote Pia wanazungumzia juu ya mkutano wa Obama na Xi Jinping .

https://p.dw.com/p/18mmc
Aliefichukua kashfa ya mawasiliano ya mtandao kudakizwa na shirika la ujasusi nchini Marekani, Edward Snowden
Aliefichua kasha ya mawasiliano ya mtandao kudakizwa na shirika la ujasusi nchini Marekani ,Edward SnowdenPicha: Reuters/Ewen MacAskill/The Guardian/Handout

 Gazeti la"Landeszeitung" linakumbusha kauli ya hapo awali, kwamba mawasiliano  ya mtandao wa internet yanapaswa kuwa njia ya mawasiliano bila ya kuwapo vipingamizi vyovyote. Lakini sasa njia hiyo imegeuzwa kuwa chombo cha upelelezi na shirika la ujasusi la Marekani.  Mhariri wa gazeti hilo anasema kufichuliwa kwa kashfa hiyo kunathibitisha kwamba, njia ya kuelekea katika nchi ambamo watu wanamulikwa kikamilifu na mashirika ya  ujasusi ni fupi sana.

Naye mhariri wa gazeti la "Hamburger Abendblatt" anasema kashfa hiyo inalichafua jina la Rais Obama,ambae ni mshindi wa nishani ya amani ya Nobel .

Mhariri huyo anealeza kwamba hakuna sababu inayoweza kuhalalisha upelelezi wa kiwango hicho, ya kuutegesha mtandao wa dunia nzima  kwa lengo la kuyadukua mawasiliano ya jamii nzima. Kwani mtandao huo unasadia nini? Mbona Marekani  haikuweza kuyaepusha mashambulio ya Boston na wala Marekani haijaweza   kuufanya usalama wa askari wake nchini Afghanistan kuwa mkubwa zaidi?

Mkutano wa kilele  wa Obama na Xi Jinping:
Gazeti la" Berliner Zeitung" linauzingatia mkutano wa siku mbili wa Marais, Xi Jinping na Barack Obama uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.Mhariri wa gazeti hilo anasema Marekani na China si marafiki wala maadui .Lakini kiuchumi nchi hizo zinategemeana.Hali hiyo inaufanya uhusiabo baina yao uwe mgumu. Ndiyo sababu kauli zilizotolewa na Marais Obama na Xi Jinping juu ya mazungumzo yao zinapaswa kutiliwa maanani.

Wote wametoa mwito wa kuwepo ruwaza mpya ya ushirikiano baina ya nchi zao.Katika muktadha wa mazingira magumu, yaliyopo baina ya Marekani na China mwito huo wa kuanzisha muundo mpya wa ushirikiano, ni hatua muhimu sana.

Ujerumani bado imekukmbwa na mafuriko :

Gazeti la "Volksstimme" linatoa maoni juu ya maafa ya mafuriko yaliyozikumba sehemu kadhaa za Ujerumani. Mhariri wa gazeti hilo anasema hadi,sasa takwimu nyingi na historia ndefu  zimetolewa juu ya mafuriko hayo.Lakini  kinachotakiwa kutolewa  zaidi, sasa ni msaada.

Naye mhariri wa "Hannoversche Allgemeine" anasisitiza kwa kusema kwamba wanasiasa hawatasaidia kwa kukumbusha juu ya maafa yaliyotokea katika karne iliyopita. Mafuriko hayana msalie na hali ya hewa haitabadilishwa kwa kutoa  takwimu.Maafa hayo yamethibitisha kwa mara nyingine kwamba waokoaji na watoaji fedha wataendelea kuhitajika.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Abdul-Rahman