1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Ugiriki na kashfa ya upelelezi

Abdu Said Mtullya17 Julai 2013

Wahariri wa magazeti wanatoa maoni juu ya Ugiriki na juu ya mvutano baina ya serikali na wapinzani nchini Ujerumani kuhusiana na mpango wa upelelezi wa Marekani.

https://p.dw.com/p/199ZI
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble -maandamano yamsubiri Athens
Waziri wa fedha wa Ujerumani ,Wolfgang Schäuble ,maandamano yamsubiri AthensPicha: Getty Images

Jumuiya za wafanyakazi zimeitisha mgomo wa nchi nzima ili kupinga hatua za kubana matumizi katika sekta ya utumishi wa serikali kwa kuwapunguza wafanyakazi katika sekta hiyo. Mhariri wa gazeti la "Der Münchner Merkur anatoa maoni kwa kueleza kuwa Wagiriki wanapita katika nyakati ngumu, kwani wanapaswa kufanya mageuzi magumu.Hata hivyo mhariri huyo anasema kuwa wafanyakazi alfu 15 katika sekta ya umma hawataachishwa hadi mwaka ujao.Mhariri huyo anakumbusha kwamba katika sekta ya watu binafsi maalfu ya nafasi za ajira zimefyekwa.

Lakini mhariri wa gazeti la "Nürnberger Nachrichten" anaziunga mkono jumuiya za wafanyakazi za nchini Ugiriki kwa kuitisha mgomo wa nchi nzima.Mhariri huyo anaeleza kuwa mipango mipya ya kubana matumizi nchini Ugiriki ni ya kushangaza.Sasa shule zinafungwa na waalimu wanapaswa kuachishwa kazi.Ni vigumu kwa mtu kuyaelewa hayo.Na wote wanaohusika wananyaa kimya-Umoja wa Ulaya Shirika la Fedha la Kimataifa,Ujerumani na wengine. Wanachotaka ni kuyaona mageuzi yakifanyika nchini Ugiriki. Lakini madhara yatakuwa makubwa zaidi. Njia hiyo italielekeza bara la Ulaya mahala pabaya.

Ziara ya Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble nchini Ugiriki:

Gazeti la"Badischen Neuesten Nachrichten" pia limeandika maoni juu ya Ugiriki , katika muktadha wa ziara Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble. Gazeti hilo linasema watu wa Ugiriki hawamtaki Waziri Schäuble.Waziri huyo atapokewa kwa maandamano mjini Athens.Kansela wa Ujerumani pia anaijua vizuri hali hiyo-kwani ameshaziona ghadhabu za watu wa Ugiriki. Na sasa Wagiriki wamempata mtu mwengine wa kumtolea hasira zao -yaani Waziri huyo wa Ujerumani.

Lakini hasira hizo zinaelekezwa mahala pasipostahili.Badala ya kuzielekeza kwa serikali yao isiyokuwa na uwezo,na kwa viongozi fisadi,vyombo vya habari na jumuiya za wafanyakazi nchini Ugiriki zinawasakama wale wanaojaribu kusaidia.

Wapinzani walalamika juu ya Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Hans-Peter Friedrich:
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Hans - Peter Friedrich alifanya ziara nchini Marekani kuhusiana na kashfa ya upelelezi uliofanywa na mashirika ya Marekani. Wapinzani wa serikali wanalalamika juu ya waziri huyo.

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" linasema wapinzani wanatangaza kuwa waziri huyo amerudi mikono mitupu kutoka Marekani. Lawama zinazotolewa na wapinzani juu ya serikali na madai ya wapinzani kwamba Kansela Merkel amekiuka kiapo chake ni mambo yaliyojulikana tokea mwanzoni kabisa. Na kwa kweli mtu hatarajii kulisikia jingine katika nyakati hizi za kampeni za uchagauzi. Lakini licha ya malalamiko hayo kutolewa na wapinzani wa serikali wakati huu wa kampeni za uchaguzi, ipo haja ya kuwaambia Wamarekani wazifuate sheria zinazotumika nchini Ujerumani.

Mwandishi :Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman