1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Ukraine

Abdu Said Mtullya5 Desemba 2013

Wahariri wanatoa maoni juu ya mgogoro wa Ukraine,ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana barani Ulaya na juu ya udanganyifu wa mabenki

https://p.dw.com/p/1ATKU
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle na Wladmir Klitschko mjini Kiew
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle na Wladmir Klitschko mjini KievPicha: GENYA SAVILOV/AFP/Getty Images

Gazeti la "Lausitzer Rundschau" limeandika juu ya ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle nchini Ukraine. Katika ziara hiyo Waziri Westerwelle alienda kwenye uwanja wa maandamano mjini Kiev na kukutana na viongozi wa upinzani.

Juu ya hatua hiyo mhariri wa "Lausitzer Rundschau" anasema kuwa Westerwelle anauelewa vizuri umuhimu wa Ukraine kwa Umoja wa Ulaya na pia anauelewa umuhimu wa kuutatua mvutano na Urusi kuhusu mkataba wa kuzishirikisha nchi za Ulaya ya mashariki katika Umoja wa Ulaya. Ansema ni kweli kwamba ni wapinzani wenyewe nchini Ukraine wanaopaswa kuyafanikisha mapinduzi waliyoyaanzisha.

Lakini mhariri wa gazeti la "Lausitzer Rundschau" anasema, pia ni kweli kwamba wapinzani nchini Ukraine wanahitaji kuungwa mkono. Na hakuna mwenye uzito zaidi katika kuwaunga mkono wapinzani hao kuliko mwakilishi wa ngazi za juu kutoka serikali ya Ujerumani.

Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana

Gazeti la Mittelbayerische" linatoa maoni juu ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wa Ulaya. Mhariri wa gazeti hilo anazielekeza lawama kwa Umoja wa Ulaya na anasema kwamba katika juhudi za kupambana na ukosefu wa ajira, Umoja wa Ulaya unajiwikea viunzi katika njia. Kosa la kwanza la Umoja wa Ulaya ni kuyaweka masuala ya ajira nje ya mamlaka yake. Halmashauri ya Umoja huo inaweza kutoa mapendekezo , lakini kujibiwa kwa mapandekezo hayo kunahitaji hiyari ya nchi wanachama. Utaratibu huo unaifanya mipano yote iwe migumu, pamoja na ule unaohusu kuwapa vijana uhakika wa maisha yao ya siku za usoni.

Hata hivyo mhariri wa gazeti la"Mittelbayerische" anasema katika maoni yake kwamba katika kipindi cha miaka saba ijayo mifuko ya Umoja wa Ulaya itajaa pomoni, kwa ajili ya miradi ya kuwaendeleza vijana. Kilichobakia sasa ni kuitumia mifuko hiyo.

Kashfa ya mabenki

Mabenki kadhaa muhimu duniani yametozwa faini ya jumla ya Euro Bilioni 1.7 kwa sababu ya kufanya udanganyifu wa viwango vya riba.Mabenki hayo yamechuma faida kubwa kutokana na njama hizo.

Juu ya kashfa hiyo gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linasema ni rahisi kuziondosha athari za kifedha, lakini siyo rahisi kuyaondosha madhara yaliyotokea katika sifa ya mabenki.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen:

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman