1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri wa magazeti juu ya Pakistan na Afghanistan.

Abdu Said Mtullya17 Agosti 2010

Wahariri wa magezi ya Ujerumani leo wanatoa maoni yao juu ya adhabu ya kifo kwa kupigwa mawe nchini Afghanistan:

https://p.dw.com/p/OpJj
Wataliban wanaotoa amri ya kuwaua wapendanao kwa kuwapiga mawe.Picha: picture-alliance/ dpa

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanatoa maoni yao juu ya maafa ya mafuriko nchini Pakistan ,mustakabal wa Afghanistan na juu ya ukatili wa taliban.

Gazeti la Hannoversche Allgemeine linatoa maoni juu ya adhabu liyotolewa na wataliban ya kuwaua watu wawili kwa kuwapiga mawe, ati kwa sababu walifanya mapenzi bila ya kuoana.

Mhariri wa gazeti hilo anasema wataliban hawakuwaua watu hao ili kutoa onyo kwa wananchi wa Afghanistan bali pia, unyama walioufanya una lengo la kutoa ishara kwa nchi za magharibi, kwamba wanao uwezo wa kufanya watakalo
Hata hivyo mhariri wa gazeti hilo anatilia maanani kwamba,mkakati wa taliban wa kutumia njia za kikatili kuwatisha wananchi umeonyesha sura yao halisi duniani kote. Na kwa haki kabisa, watu wanauliza, jee hao taliban ndiyo watu wa kuitawala Afghanistan?

Gazeti la Weser-Kurier pia linazungumzia juu ya mustakabal wa Afghanistan. Na linauliza nini kitatokea ikiwa majeshi ya kimataifa yanayolinda amani yataondoka nchini humo?

Mhariri wa gazeti hilo anajibu swali hilo kwa kueleza kwamba,wanaitikadi kali wa kiislam yaani taliban, hawatarudi nyuma katika matendo yao ya ukatili.Siyo tu kwamba wataendelea kuwapiga mawe na kuwaua watu wanaopendana , bali pia watataka kuondolewa majeshi ya nchi zote 42 yanayopambana na taliban.Na hiyo wataitumia kama ishara ya kuonyesha kwamba wao ni watu wasioshindika.Ishara hiyo itakuwa shinikizo kwa nchi za kiislamu zenye mtazamo wa ukadirufu kama zile za ghuba.

Na ndiyo sababu ,mhariri wa gazeti la Weser-Kurier anauunga mkono msimamo wa Kamanda Mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, jenerali David Petraeus kwamba muda mrefu zaidi utahitajika ili kuleta mafanikio nchini Afghanistan.

Gazeti la Mittelbayarische pia linazungumzia hali ya Afghanistan, kwa kuzitanabahisha nchi za magharibi juu ya vita vya propaganda. Gazeti hilo linafafanua kwa kusema kwamba nchi za magharibi zinaonyesha picha za watu wanaouawa kikatili nchini Afghanistan ,ili kuthibitisha umuhimu wa kuendelea na vita hivyo. Lakini mhariri wa gazeti hilo anasema, picha hizo zinaweletea manufaa taliban tu.

Sababu ni kwamba kila raia anaeuawa na majeshi ya Nato kwa bahati mbaya, ni ushindi kwa taliban.

PAKISTAN:
Mamia ya watu wamekufa na mamilioni wengine wameathirika kutokana na maafa ya mafuriko nchini Pakistan.

Juu ya maafa hayo gazeti la Kieler Nachrichten linasema,ikiwa jumuiya ya kimataifa haitaisaidia serikali ya Pakistan, wanaitikadi kali wa kiislamu watayatumia maafa hayo kwa manufaa yao ya kisiasa.

Gazeti hilo linaeleza:

"Maafa yaliyoifika Pakistan yanatuonyesha jambo moja dhahiri, kwamba licha ya kauli za kuvutia, dunia imegawanyika .Lakini lazima jumuiya ya kimataifa isimame pamoja, la sivyo mamilioni ya wale walioathirika na mafuriko watakimbilia kwa watu wenye siasa kali."

Mwandishi/ Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/

Mhariri/.. Josephat Charo