1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri wa magazeti

15 Machi 2007

Baraza la mawaziri la Ujerumani limepiga hatua nyingine muhimu katika mpango wake wa mageuzi kwa kupitisha kodi ya wajasir -amali. Katika maoni yao ,wahariri wa magazeti leo wanazingtia umuhimu wa hatua hiyo

https://p.dw.com/p/CHTU

Mhariri wa gazeti la REUITLINGER-GENERAL ANZEIGER anasema kuwa uamuzi wa serikali juu ya kupunguza kodi kwa wajasiramali ni habari nzuri kwa uchumi wa nchi.

Kodi hiyo itapunguzwa hadi kufikia asilimia 30 yaani punguzo la asilimia 8.

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa uamuzi huo utatoa mchango katika kudumisha nafasi za ajira licha ya jumuiya za wafanyakazi kuwa na mtazamo tofauti.

Gazeti linatilia maanani kuwa , kuanzia Irland hadi Ulaya mashariki, kodi ya viwanda ilipunguzwa miaka mingi iliyopota.

Lakini mhariri wa gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG anashauri kuwapo tahadhari, juu ya uamuzi huo. Gazeti linakumbusha juu ya hatua nyingine ya mageuzi iliyopitishwa katika sekta ya afya iliyosababisha patashika katika jamii .

Gazeti la EXPRESS la mjini Cologne linasisitiza kuwa unafuu wa kodi kwa makampuni utaifanya Ujerumani iwe nchi ya kuvutia kibiashara , na hasa sasa wakati ambapo uchumi unastawi vizuri.

Gazeti hilo linasema , lazima ifahamike kwamba Ujerumani haipo peke yake duniani. Katika nchi zingine vilevile fedha zinaingizwa, pia kutokana na kupunguza kodi.

Katika maoni yake gazeti maarufu FRANKFURTER RUNDSCHAU linakumbusha kwamba tokea siku ya kwanza mradi huo wa kupunguza kodi ulikuwa unatiliwa mashaka na wajumbe wa chama cha Sozial demkoratik kilichomo katika serikali ya mseto. Wajumbe wa chama hicho walikuwa wanahoji , kuwa kuwapunguzia kodi matajiri ni jambo gumu kueleweka. Na hivyo basi ni jambo la kufurahisha zaidi kuona kwamba mradi huo umepitishwa pia na waziri wa fedha bwana Steinbrück wa chama hicho

Mhariri wa gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN pia anatilia maanani kuwa kodi ya wajasiramali inapunguzwa wakati ambapo makampuni yanazoa faida kubwa kubwa. Na pamoja na wengine , megeuzi hayo yamepitishwa pia na waziri na fedha ambae ni mwanachama wa chama cha sozial demokratik kinachojiita kuwa ni chama cha watu wadogo.

Mhariri anatamka kuwa kwa jumla uamuzi wa kupunguza kodi ni sahihi kabisa,japo mhariri wa gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND anasema kuwa uamuzi huo ni muhali, kwa baadhi ya wanachama wa Social Demokratik.

Na gazeti la BERLINER ZEITUNG linaeleza , kuwa watakaonufaika na uamuzi wa kupunguza kodi, ni makampuni makubwa . Gazeti hilo linasikitika katika maoni yake kwamba viwanda na makapuni ya kati hayajafanyiwa, kinachoweza kuonekana dhahiri kwa manufaa yao , katika mchakato wote wa mageuzi.

Na mhiriri wa OSTTHÜRINGER anawaonya wale wanaotathmini kinyume kabisa, shabaha za kuleta haki. Mhariri wa gazeti hilo anasema katika maoni yake kwamba yeyote anaepinga uamuzi muhimu kama huo wa kupunguza kodi , ajue kwamba anavuruga kila kitu na hasa ustawi wa uchumi unaomnufaisha kila mwananchi.