1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 30 baada ya ajali ya Chernobyl

26 Aprili 2016

Wahariri leo wanatoa maoni juu ya maafa ya nyuklia yaliyotukia nchini Ukraine miaka 30 iliyopita.Pia wananaizungumzia ziara ya Rais Obama barani Ulaya

https://p.dw.com/p/1Icjq
Picha: picture-alliance/dpa/M.Markiv/Press Office of the President of Ukraine

Miaka 30 iliyopita ajali mbaya sana ya nyuklia ilitukia katika mji wa Chernobyl wa nchini Ukraine. Maalfu ya watu walikufa kutokana na athari za ajali hiyo na kuzilazimisha serikali kuwa na mtazamo mpya juu ya nishati ya nyuklia.

Katika kuyakumbuka maafa hayo leo, mhariri wa gazeti la "Mittelbayerische" anaisifu sera ya Ujerumani. Anatilia maanani kwamba katika nchi nyingi za viwanda sekta ya nishati ya nyuklia inahaulishwa.

Hata hivyo katika nchi nyingine serikali zinawakilisha sera inayokubali ajali kama zile zilizotukia Chernobyl na Fukushima mradi zinatukia kila baada ya robo karne.

Merkel asifiwa kufuata sera nzuri ya nishati ya nyuklia

Ndiyo sababu mhariri wa gazeti la "Mittelbayerische" anaisifu serikali ya Ujerumani kwa kuondokana kabisa na sera hiyo ya hatari.Mhariri huyo anatilia maanani kwamba Kansela wa Ujerumani anapinga katu katu nishati ya nyuklia nchini.

Lakini gazeti linasema si Angela Merkel peke yake anaestashili sifa. Wanaharakati waliopinga nishati ya nyuklia kwa miongo kadhaa pia wanastahili sifa.Mhariri wa "Mittelbayerische" anasema ni kutokana na kampeni za wanaharakati hao kwamba Ujerumani ilipitisha sera ya mageuzi katika sekta ya nishati.

Rais Poroshenko awarehemu waliokumbwa na maafa ya nyuklia
Rais Poroshenko awarehemu waliokumbwa na maafa ya nyukliaPicha: picture-alliance/dpa/M.Markiv/Press Office of the President of Ukraine

Gazeti la "Braunschweiger " linaizungumzia hotuba ya Rais Barack Obama aliyoitoa katika mji wa Hannover .Katika hotuba hiyo Obama alizungumzia juu ya mustakabal wa bara la Ulaya. Mhariri huyo anaeleza kuwa Obama aliwahutubia vijana na chipukizi yaani warithi wa kesho. Na ikiwa aliweza kuwapa vijana hao uhakika, basi ametoa huduma muhimu kwa bara la Ulaya. Hata hivyo alipaswa pia kuzitembelea nchi ambako moyo wa Ulaya ya pamoja unafifia.


Gazeti la "Südwest -Presse" linawataka viongozi wa Ulaya na Marekani wazingatie tofauti zilizopo za ukale na usasa,kuhusu mkataba wa biashara huru ,baina ya pande hizo mbili. Mhariri wa gazeti hilo anahoji kwamba Rais Obama na Kansela Merkel wanakubaliana jambo moja kuhusu mkataba wa biashara huru , baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya ,TTIP

Mambo yatakuwa mazuri kwa wafanyakazi,wanunuzi na kwa mazingira. Wawekaji vitega uchumi pia watanufaika. Lakini barani,Ulaya mkazo unawekwa katika kulinda afya za watu. Na nchini Marekani, hatua zinachukuliwa ikiwa kwanza pana ushahidi.

Ndiyo sababu, mhariri anasema mkataba wa biashara huru baina ya Marekani na Ulaya utakubalika ikiwa tu tofauti zilizopo baina ya pande mbili hizo zitazingatiwa.

Mwandishi:Mtullya abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman