1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri

2 Julai 2007

Katika safu zao za maoni wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya majaribio ya mashambulio ya kigaidi nchini Uingereza .

https://p.dw.com/p/CHSY

Katika maoni yao wahariri hao pia wanazungumzia juu ya mgomo wa wafanyakazi wa reli hapa nchini .

Juu ya yalitokea katika miji ya London na Glasgow mhariri wa gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU anasema kuwa watu nchini Uingereza wamebahatika kwa kuwa wamenusurika maangamizi . Magaidi hawakufanikiwa katika shabaha zao. Lakini wamefanikiwa kuwaweka watu katika hali ya taharuki, hali ya wasiwasi barani Ulaya kote.Mhariri huyo anasema kuwa wasiwasi huo unazidi kuwa mkubwa.Kutokana na hali hiyo mhariri wa gazeti anatabiri kuwa watu wa Ulaya sasa watazitaka serikali zao ziimarishe zaidi usalama .


Katika maoni yake mhariri wa gazeti la KIELER NACHRICHTEN anasisitiza mambo mawili katika kupambana na changamoto ya ugaidi. Utulivu na kuwa macho.

Mhariri anasema changamoto ya kupambana na ugaidi siyo jukumu la wanajeshi na polisi peke yao. Gazeti linaeleza kuwa harakati za kupambana na ugaidi zinalazimu mkakati wa kugusa akili na mioyo ya watu.


Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linatahadharisha kuwa , yaliyotokea nchini Uingereza siyo suala la waingereza peke yao.Mhariri wa gazeti hilo anasema litakuwa kosa kufikiri kwamba majaribio yayaliyofanywa na magaidi hayana uhusiano na matukio mengine duniani.

Mhariri huyo anakumbusha vita vya Irak ambapo Uingereza pia inashiriki . Kwa hiyo jaribio la magaidi ni mtihani wa kwanza kwa waziri mkuu mpya Gordon Brown.


Wahariri leo pia wanazungumzia juu ya tishio la mgomo la wafanyakazi wa shirika la reli.Takriban wote wanasema kuwa madai ya wafanyakazi wa shirika la reli ni wendawazimu.Wafanyakazi hao wanataka nyongeza ya asilimia 31 katika mishahara yao!

Juu ya hayo mhariri wa gazeti la SCHWARZWÄLDER BOTE anaitahadharisha jumuiya ya madereva wa treni . Anaikumbusha jumuiya hiyo kwamba kutokana na usumbufu unaosababishwa na mgomo ,wateja wanaweza kuamua kupanda ndege za bei nafuu.

Mhariri wa gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG pia anasisitiza hayo hayo katika maoni yake.

Hasa wakati huu wa likizo hapa nchini Ujerumani mgomo huo ni usumbufu kwa wateja, Hiyvo basi wanaweza kuamua kupanda ndege ama kutumia magari yao. Pande zote mbili, mwajiri na mwajiriwa zinapaswa kutambua hayo.

AM