1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri

A.Mtullya20 Novemba 2007

Maoni ya wahariri. Viongozi wa jumuiya ya wafanyakazi na wa shirika la reli wamezungumza ana kwa ana juu ya kumaliza mgomo wa madereva wa treni hapa nchini.

https://p.dw.com/p/CP1s

Mgomo huo ni wa madereva wa treni wa shirika la reli la Ujerumani . Madereva hao wanadai nyongeza ya mshahara ya hadi asilimia 30. Mgomo huo umeshachukua siku kadhaa ukifanyika hatua kwa hatua.

Na sasa viongozi wa jumuiya ya wafanyakazi na wa mwajiri yaani shirika la reli wameanza tena kuwasiliana ana kwa kwa ana.

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linasema waziri wa usafirishaji Tiefensee amedokeza matumaini juu ya kumalizika mgogoro huo kwa kusema kuwa meneja wa kampuni ya reli yupo tayari kusogea hatua moja na kutoa pendekezo kwa jumuiya ya wafanyakazi inayowawakilisha madereva.

Lakini mhariri wa gazeti hilo anasema mwajiri- yaani shirika la reli limebanza kimya.

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linatilia maanani kuwa katika baraza la uongozi la shirika hilo wapo wajumbe ambao wakati wote wamekuwa wanawakilisha msimamo mkali dhidi ya madereva;gazeti linaeleza kuwa lengo la wajumbe hao kufanya hivyo, ni kutowashtua watu wanaotaka kununua sehemu ya shirika hilo.

Kwani kuna mipango ya kulibinafsisha shirika hilo. Lakini gazeti linasema mgomo wa madereva lazima uwe umemalizika hadi itakapofika krismasi!

Mhariri wa gazeti la FRÄNKISCHE TAG anasema wanaoweza kumaliza mgomo huo ni meneja wa shirika la reli na mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyakazi inayowalikisha maslahi ya madereva.

Walakini mhariri wa gazeti hilo katika maoni yake anasema pande mbili hizo zinaweza kufikia usikizano juu ya mishahara japo mhariri huyo pia anasisitiza kuwa madai ya nyongeza ya asilimia zaidi ya 20 yanathibitisha kuwa jumuiya ya wafanyakazi imekuwa usingizini kwa muda wa miaka mingi.

Gazeti linasema pande mbili hizo zinapaswa kutatua mgogoro wao ili zipate wasaa wa kushughulikia suala la kulibinafshisha shirika.

Katika maoni yake gazeti la TEGESSPIEGEL linakumbusha juu ya hasara iliyosababishwa na mgomo huo na kusema , hapakuwa na ulazima wa hali kufikia kiwango hicho.

Mharriri anasema mamilioni ya wasafiri wamekasirishwa na mgomo huo na wamepoteza imani juu ya shirika la reli-sambamba na hayo uchumi umeingia hasara. Gazeti linasema , hayo hayakuwa lazima, kwani msingi wa mazungumzo juu ya kutatua mgogoro huo umekuwapo siku nyingi.

Na hakika inawezekana kufikia suluhisho hadi itakapofikia krismasi.

Lakini gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linasema alichotarajia mwajiri hakikujiri!

Mwajiri alifikiri kuwa wasafiri wasingekuwa tena na stahamala juu ya madereva wa treni na kwamba madereva hao wangelilazimika kukubali mapendekezo ya mwajiri. Lakini hayo hayakuwa hivyo.

Madereva wanandelea na mgomo na mwajiri pia anaendelea kuwa na msimamo mkali. Gazeti linasema matumaini ya kufikiwa suluhisho bado yapo mbali.