1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya walimwengu baada ya Annapolis

Oummilkheir28 Novemba 2007

Shaka shaka zimejaa licha ya matumaini ya kufikiwa amani Mashariki ya kati

https://p.dw.com/p/CUFY
Maandamano dhidi ya mkutano wa AnnapolisPicha: AP

Hisia tofauti zimeenea mashariki ya kati,baada ya mkutano wa kimataifa wa Annapolis.Waarabu na waisrael wanashuku kama viongozi wao watakua na muda wa kutosha kufikia makubaliano hadi mwisho wa mwaka 2008.Lakini kuna wengine pia wanaohisi Annapolis ilikua kazi bure.

Kwa upande wa waisrael,shaka shaka zimetanda zaidi katika vyombo vya habari kama kweli muda huo utaheshimiwa.Magazeti yanakumbusha matamshi ya waziri mkuu wa zamani,marehemu Yitzhak Rabin aliyewahi kusema ”Mashariki ya kati hakuna tarehe iliyotukuka.”

Hanan Cristal,mhariri wa Radio ya taifa anahisi kwa hivyo,hotuba ya waziri mkuu Ehud Olmert haikua na uzito wowote kwa namna ambayo chama cha siasa kali za kizalendo Israel Beitenou na kile cha itikadi kali cha Shas vimeamua kusalia katika serikali ya muungano.

“ Ehud Olmert amejipatia mwaka mmoja zaidi” anasema Cristal,akisisitiza waziri mkuu hajaridhia hata kidogo yanapohusika na masuala muhimu mfano kanuni za Jerusalem ya Mashariki,wakimbizi wa kipalastina au mipaka ya taifa la siku za mbele la wapalastina.

“Yaliyotokea Annapolis hayana umuhimu wowote” amesema kwa upande wake waziri wa mikakati Avigor Liebermann,ambnae pia ni mwemyekiti wa chama cha Israel Beitenou.

Waziri wa biashara na viwanda Eli Yishai,mmojawapo wa viongozi wa Shass anafungamanisha mkutano wa Annapolis na “ndoto” akisema kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas ni mshirika wa kubuni tuu,na hana usemi wowote Gaza-eneo linalodhibitiwa na Hamas tangu June iliyopita.

Bwana mmoja wa kiyahudi anasema

“Abu Mazen hajatumwa,Bush hajatumwa,Olmert hajatumwa.”Sasa vipi watu watafanikiwa?”

Kwa upande wa wahamiaji wa kiyahudi,hakuna sauti iliyosikika.WEnyewe wanahisi maandamano na duwa walizoomba jumatatu iliyopita,mkutano wa Annapolis ushindwe,zitakubaliwa.

Kwa upande wa wapalastina,gazeti la Al Qodos linaloelemea zaidi upande wa chama acha Mahmpud Abbas-Fatah,linahisi Annapolis ni hatua ya kutia moyo-japo kama huu ni mwanzo tuu.”Mkutano huu umewatupia mpira waisrael na kuipatia fursa Marekani iwashinikize viongozi wa Israel wachangie kwa moyo mkunjufu katika utaratibu wa amani.Al Hayat gazeti la utawala wa ndani wa palastina linasema idadi kubwa ya wapalastina wanaunga mkono utaratibu wa amani.

Hamas,wanaopinga mazungumzo ya Annapolis ,na kufika hadi ya kusema Mahmoud Abbas hana haki ya kuzungumza kwa niaba ya wapalastina,wanasema Annapolisi ilikua kazi bure.

Rais Mahmoud Ahmedinedjad wa Iran,mpinzani mwengine mkubwa wa mazungumzo ya amani kati ya waarabu na Israel,amesema hii leo tunanukuu”Israel haitanusurika na mkutano wa Annapolis hauna maana yoyote.Mwisho wa kumnukuu.

Wakati huo huo vikosi vya usalama,tiifu kwa rais Mahmoud Abbas,vimefyetua risasi hii leo huko Herbrone wakati wa maandamano kupinga mkutano wa Annapolis.Watu kadhaa wamejeruhiwa.Wanajeshi hao wamejibisha hujuma za mawe waliyovurumishiwa na watu waliokua wakishiriki katika mazishi ya mwanaharakati mmoja aliyeuliwa jana Hebrone.Watu kadhaa wamekamatwa na bendera za Hamas kuchukuliwa.