1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni:Merkel aendelee kwa mtazamo tofauti

23 Septemba 2013

Kansela Merkel ataendelea kutawala hilo ni wazi. Hata hivyo serikali aliyokuwa akiiongoza itabadilika, kwa maana ya vyama vitakavyokuwa katika mseto wa serikali.

https://p.dw.com/p/19mBP
Ute Schaeffer, Deutsche Welle, Chefredakteurin, Multimediadirektion Regionen, Editor in chief, Multimedia Regions Department. Foto: DW/Per Henriksen 27.07.2012. DW2_3666.
Mhariri Mkuu wa Deutsche Welle, Ute SchaefferPicha: DW/P. Henriksen

Mamlaka ya kuiongoza serikali yatakuwa mikononi mwa Merkel, chama chake cha Christian Democratic Union, CDU, kimepata asilimia 42 ya kura na kuwa chama chenye wingi mkubwa katika bunge la Ujerumani, Bundestag. Lakini chama cha kiliberali FDP kimepotea njia.

Inaonekana kuwa katika muda wa miaka minne ijayo chama kitakachoiongoza Ujerumani ni cha Christian Democratic, ama kwa ushirikiano wa pamoja na chama cha Social Democratic ama kitaweza kufanya hivyo peke yake.

Mafanikio ya kansela

Mambo ambayo ameyafanya kansela Merkel yamekuwa si rahisi kuyakiuka, na chama chake cha CDU, kimefaidika na mtazamo huo wa mgombea wake. Ni mafanikio makubwa kabisa katika uchaguzi katika miongo miwili iliyopita. Matokeo hayo ya uchaguzi hata hivyo yamekuja na muanguko wa kihistoria wa chama kidogo mshirika katika serikali iliyopita ya Merkel.

Chama cha FDP kilipata matokeo mazuri ya asilimia 14 miaka minne iliyopita na kuingia katika serikali, lakini hivi sasa hakitakuwamo katika bunge la Ujerumani. Muanguko mkubwa wa chama hicho ni mabadiliko makubwa katika medali ya siasa nchini Ujerumani, kwasababu tangu kuundwa kwa jamhuri ya Ujerumani mwaka 1949 chama hicho kimekuwa na uwakilishi katika bunge.

Ni wazi kabisa kuwa mafanikio ya muungano wa serikali yalikuwa mafanikio ya kansela Merkel. Ujerumani ina idadi ndogo kabisa ya watu wasio na ajira katika Ulaya , ukuaji imara wa uchumi , na deni dogo la serikali. Na haya yote yamekuja bila ya kupitia kipindi kigumu kwa Wajerumani wengi. Haya yote yamewavutia wapiga kura. Wanataka kuendelea na hali hiyo, uthabiti na usalama. Na hivyo kumrejesha madarakani kansela Angela Merkel. Baada ya miaka minane madarakani , amekuwa dhahiri mwanasiasa mwanamke mwenye madaraka makubwa.

Sera muhimu

Kwa hiyo anadhibiti sera muhimu za upande wa upinzani. Haki zaidi za kijamii. Misaada kwa familia. Kuondoa sheria ya kutumikia jeshi kwa mujibu wa sheria. Kutojiingiza nchini Libya ama Syria . Kuongoza mabadiliko ya sekta ya nishati. Muungano uliotawala miaka minne iliyopita karatasini ulikuwa ni muungano wa wananchi, lakini ulitawala kwa mada nyingi kutoka katika sera za Social Democratic, na hususan sera za chama cha kijani. Nadharia halisi ya vitendo. Hiyo ndio msingi wa Merkel na unaelekea kuwa ni maarufu.

Kwa Merkel , na hususan kwa wafuasi wake , kuimarisha kazi zake za kisiasa katika muungano mkuu halitakuwa tatizo. Kinyume chake , pamoja na chama cha Social Democratic, hali ya mvutano uliokuwapo kutokana na udhibiti wa vyama vya SPD na kijani katika bunge la wawakilishi wa majimbo , Bundesrat utakuwa mwepesi zaidi kuudhibiti. Vyama hivyo kwa sasa vimezuwia sheria muhimu kupita katika bunge hilo. Medani ya siasa nchini Ujerumani imeanza kubadilika. Ushirika umebadilika.

Vyama havijaridhika na matokeo

Chama cha SPD na kijani havijaridhika na matokeo yake ya uchaguzi. Pamoja na hayo juhudi za mgombea wa chama cha SPD Peer Steinbrück katika wiki za mwisho kuweza kupata kura nyingi iwezekanavyo katika uchaguzi huo, zimewezesha chama hicho kupata alama tatu tu zaidi na kufikisha asilimia 26. Hizi ni chache kuliko ilivyotarajiwa. Chama cha SPD kilipambana kulinda hadhi yake kama chama cha wananchi.

Hii ni kwamba , mada zake za misaada kwa jamii zimechukuliwa na kansela Merkel na kuzitekeleza. Na kwa upande mwingine sera zake hazikuwavutia wapiga kura wengi. Kwa robo karne baada ya muungano wa Ujerumani mbili chama cha Die Linke , kinakuwa chama kinachofuatia na kuweza kuchomoza kutoka katika chama kilichokuwa cha kisoshalist cha Ujerumani ya mashariki ya zamani cha SED, na kuwa chama cha tatu kwa ukubwa katika Ujerumani.

Chama kilichojitenga cha Alternative für Deutschland, chama mbadala kwa Ujerumani AfD, kimejionesha kuwa kinatambuliwa. Chama hicho kinachopinga sarafu ya euro kimepata kuungwa mkono na watu wanaopinga , lakini hakina mwelekeo na kimefadhaisha katika maeneo yote ya kisiasa.

Mwandishi: Ute Schaeffer/ZR/Sekione Kitojo

Mhariri: Idd Ssessanga