1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni:Mkutano kuhusu Syria usio na umuhimu?

Josephat Nyiro Charo29 Oktoba 2014

Mkutano kuhusu wakimbizi wa Syria uliofanyika Berlin haukuhusu utoaji wa ahadi za kifedha, lakini katika maoni yake mwandishi wa DW Dagmer Engel anatoa sababu kumi kwa nini mkutano huo ungeweza kuwa na umuhimu.

https://p.dw.com/p/1DddI
Kommentarfoto Dagmar Engel Hauptstadtstudio
Picha: DW/S. Eichberg

Mkutano uliojadili hali ya wakimbizi wa Syria ulioandaliwa na Ujerumani umekamilika mjini Berlin huku Ujerumani ikiahidi kutoa kiasi cha euro milioni 500 kwa ajili ya wakimbizi hao.

Nje ya eneo la machafuko nchini Syria janga la wakimbizi lilikuwa tayari karibu limeshasahaulika. Mapambano dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu yamezigubika taarifa nyingine zote kutoka eneo hilo.

Sasa imetambulika kwamba wakimbizi hao sio watu pekee wanaokabiliwa na hali ngumu. Nchi zinazowachukua pia zinahitaji msaada wa haraka.

Kilio cha kutaka msaada kutoka nchi jirani na Syria hakijawahi kusikika kama ilivyotokea katika mkutano wa Berlin. Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Lebanon na Jordan walitoa miito yenye hamasa kuhusu hali tete nchini mwao.

Ilihamasisha kufahamu juu ya utayarifu wa kujitolea nchi hizi mbili ndogo zinazouonyesha kwa majirani zao wanaohitaji msaada.

Wakati huo huo ni aibu kwa mapengo makubwa ya jumuiya ya kimataifa. Hii inaongeza utayarifu wa kufanya mengi zaidi kushiriki na kuzisaidia nchi zinazowapokea wakimbizi na jamii zao. Hii inaweza kusababisha hali ambapo miundombinu na utajiri unakua kwa kasi kubwa zaidi katika miji na vijiji vinavyotoa makazi kwa wakimbizi kuliko maeneo mengine katika eneo hilo.

Wakimbizi wa Syria hawatarejeshwa nchini kwao ili mradi vita vinaendelea. Serikali ya Lebanon tayari kwa muda sasa imesaidia juhudi za kuwarejesha wakimbizi katika maeneo ya Syria ambayo hayajaathiriwa sana na vita. Lakini washiriki katika mkutano wa Berlin, ikiwemo Jordan, hawakuunga mkono kabisa mpango huo.

Ujerumani inatambulika kimataifa kwa kujitolea kwake. Tayari imewachukua wakimbizi 70,000 wa Syria, idadi ambayo ni kubwa kuliko iliyochukuliwa na kila nchi nyingine ya Ulaya.

Utambuzi wa Ujerumani pia unaongeza shinikizo kwa mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya. Mjadala kuhusu wakimbizi unafufuliwa. Fedha zilizo tayari kutumika kwa ajili ya misaada huenda hatimaye zikatolewa.

Ujerumani pia imekuwa msitari wa mbele kwa kuahidi euro milioni 500 katika miaka mitatu ijayo. Fedha zitawekezwa katika miundombinu kama vile hospitali, ugavi wa maji na elimu ya watoto. Wengine pengine wataiga mfano huo.

Mkutano wa Berlin umedhihirisha viongozi hawana suluhisho, na wanalikubali hilo. Ahadi zilizotolewa kwenye mkutano wa Berlin kwa nchi zinazowapokea wakimbizi wakati huo huo ni kauli kwamba umwagikaji wa damu utaendelea nchini Syria. Kuna uaminifu katika hilo. Suluhisho la kisiasa linatafutwa, lakini haliko karibu kupatikana.

Mwandishi:Engel, Dagmer

Tafsiri:Josephat Charo

Mhariri:Sekione Kitojo