1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni:Umoja wa ulaya wasaka njia za kuitanabahisha Urusi

4 Machi 2014

Mshikamano Madhubuti kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani ndio Ngao itakayomtanabahisha Rais Vladimir Putin abadilishe Msimamo wake shupavu katika Mzozo wa Ukraine

https://p.dw.com/p/1BJGj
Mhariri wa DW Bernd RiegertPicha: DW/P. Henriksen

Azuwiliwe vipi, muimla,katili, anaetaka kutetea masilahi yake bila ya kujali kupoteza hadhi yake?Masuala hayo walijiuliza mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya na siku moja kabla, hata mabalozi wa jumuia ya kujihami ya NATO mjini Brussels.Jibu la suala si rahisi,kama watu hawataki kujibwaga katika operesheni za kijeshi na kusababisha mzozo usiokadirika.Vladimir Putin ni wa enzi za zamani kwasababu angali bado anaotea yale yaliyokuwepo wakati wa vita baridi.Kwa kuingilia Crimea Putin amebainisha wazi wazi bado anang'ang'ania maeneo ya ile iliyokuwa ikijulikana kama milki ya Usovieti,.

Putin ni afisa wa zamani wa idara ya upelelezi ya Urusi KGB,ni afisa wa ngazi ya juu chamani,mtu mwenye kiu cha madaraka,na sio mwanademokrasia na wala si mtu asiyekuwa na dosari,kama alivyodai miaka kadhaa iliyopita kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder.Hapo mtu anaweza kulalamika lakini ukweli ni kwamba Putin anaidhibiti kikamilifu Urusi .Na ndio maana watu hawana budi isipokuwa kushirikiana nae na kupatana nae ikiwa watataka kuepusha balaa lisitokee.Hisia zinasema Umoja wa Ulaya lazma uvinjari.Busara lakini zinasema watu lazma wajaribu kuituliza Urusi,kuishirikisha na kuijumuisha katika juhudi za kidiplomasia.Na hilo hasa ndilo mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa ulaya walilojaribu kulifanya walipotathmini kwanza uwezekano wa kuiwekea vikwazo na kuitolea wito Urusi ipitishe hatua za kutuliza hali ya mambo.Yatatosha? Kitatokea nini ikiwa Vladimir Putin atafuata anachokitaka mweyewe?

Malumbano au Masikilizano?

Hali hii si mpya na katika historia daima imekuwa ikijirudia:Mtawala anaivamia nchi nyengine kwasababu jamii ya walio wachache au watu wenye asili ya nchi yake eti wameomba wasaidiwe.Anaikalia sehemu ya nchi hiyo kuepusha hatari isitokee.Ilitokea hivyo hivyo mwaka 1938 Adolf Hitler alipoivamia sehemu ya Tchekoslovakia.Tusielewane vibaya,Putin hawezi kulinganishwa na Hitler.Eneo la Tchekoslovakia lenye wakaazi wenye asili ya Ujerumani,lijulikanalo kama Sudetenland,mtu hawezi kulilinganisha na Crimea.Na hali pia ni nyengine ingawa mpango unaonyesha kuwa wa aina moja.Mpango ulibainika pia mwaka 2008 pale Putin alipotuma wanajeshi kuyakalia majimbo ya Abkhasia na Ossetia nchini Georgia.Na hoja zinazotolewa hivi sasa ni zile zile eti kuwahui watu wenye asili ya Urusi huko Crimea..Kama ilivyokuwa mwaka 1938 na mwaka 2008,jumuia ya mataifa ya kidemokrasia haina jengine la kufanya ila kusubiri tu kwasababu hakuna anaetaka kuchochea hatari ya kuripuka vita kwasababu ya eneo dogo la ardhi.Na hilo rais Putin wa Urusi analitamabua fika na ndio maana ana hakika,ingawa mataifa ya kidemokrasia ya magharibi yatalalamika,na pengine vikwazo kuiwekea lakini hayatokwenda umbali wa kujibu matumizi ya nguvu kwa matumizi ya nguvu.Hali kama hiyo ilitokea pia mwaka 2008,uhusiano wa kidiplomasia ulipopooza na,mikutano kususiwa,lakini uhusiano wa kawaida pamoja na Urusi,nchi muhimu kiuchumi haujakawia .

Mshikamo Madhubuti kati ya Umoja wa ulaya na Marekani

Muhimu ni kwa Umoja wa Ulaya na Marekani kuonyesha mshikamano.Urusi ikifanikiwa kuleta mfarakano,itakayokula hasara ni Ulaya hapo.Na Umoja wa Ulaya unahitaji uungaji mkono wa Marekani kwasababu mshikamano madhubuti pekee yake ndio unaoweza kumtanabahisha Putin.

Mwandishi:Bernd Riegert/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Yusuf Saumu