1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano ya kugombea urais Ufaransa yachacha biana ya Sarkozy na Royal.

23 Aprili 2007

Nicolas Sarkozy wa chama cha kihafidhina na msosialist Segolene Royal ndio watakaopambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa.

https://p.dw.com/p/CHFg
Segolene Royal na Mpinzani wake Nicholas Sarkozy.
Segolene Royal na Mpinzani wake Nicholas Sarkozy.Picha: AP/DW

Wagombeaji hao waliwashinda wagombeaji wengine kumi katika uchaguzi ambapo zaidi ya aslimia 85 ya wapiga kura walijitokeza vituoni katika historia ya uchaguzi nchini Ufaransa.

Nicholas Sarkozy alipata asilimia 31 ya kura huku Segolene Royal akipata asilimi 26 ya kura zilizopigwa. Uchaguzi wa mwaka huu uliweka rekodi kubwa kwa sababu asilimia themanini na tano wapiga kura walijitokeza vituoni, ukio ambalo halijatokea kwa miaka arubaini sasa katika siasa nchini humo.

Na tayari mapambano baina yao yanazidi kuchacha huku baina ya wagombeaji hawa Nicholas Sarkozy na Segolene Royale.Royal Anasemekana kuwa tayari anaungwa mkono na wagombeaji 6 wa mrengo wa kushoto ambao walipata asilimia kumi ya kura zilizopigwa.

Lakini Matokeo ya uchaguzi huu yamedhihirisha wazi kuwa sasa wapiga kura watabidi wachague mbili tuu, aidha kupiga kura kwa upande wa chama cha kihafidhina cha Sarkozy au kumpigia msocialisti Segolene Royale. Wapiga kura hao wanakabiliwa na changamoto ya maamuzi yao kwani mtindo wa wagombeaji hawa ni mpya na tofauti na wagombeaji wa zamani.

Sarkozy,mwenye asili ya kihungaria, amedhihirisha msimao unaofananishwa na wamarekani na waingereza kutokana na masuala anayoibua ya wahamiaji na uchumi tofauti na marais wa zamani walioongoza Ufaransa.

Na anapingwa na mrengo wa kushoto ambao ndiyo wasocialisti wanaoogopa mabadiliko ya kutumia nguvu yatakayobadili tamaduni za Ufaransa kwa kuwalazimu kufanya kazi zaidi.

Bi segolene Royal naye,anawaahidi wafaransa kuibadilisha Ufaransa kwa utaratibu tofauti na mpinzani wake Sarkozy anayetaka kufanya mabadiliko ya haraka. Royale amelenga kizazi kipya cha Ufaransa kwa kutaka wapewe malipo mazuri,kuleta sera zitakazolinda haki za binadamu na hasa usawa kwa wahamiaji.

Changamoto yao kubwa ni kutega kura za wagombeaji walioshindwa katika uchaguzi huu wa pili utakaofanyika wiki mbili zijazo. Mojawapo ya kura hizo ni asilimia kumi na nane zilizoelekezwa kwa mgombeaji Francois Bayrou.

Mgombeaji mwengine aliyeshindwa kwa mara ya ya pili baada ya kujaribu kuogmbea uarisi mwaka 2002 ni Jean-Marie Le Pen ambaye anahisiwa kupinga sera ya Sarkozy

Kampeini zinatarajiwa kuanza tarehe 27 mwezi huu,wagombeaji hao kisha watafanya mjadla katika televisheni mwezi Mei tarehe 2 na uchaguzi kufanywa tarehe sita. Wachaunguzi wa kisiasa na wanasema huenda Sarkozy akashinda duru ya pili kwa asilimia hamsini na tano dhidi ya Segolene ambaye huenda tuu akafikisha asilimi arubaini na nane lakini ikiwa tuu wataweza kuwashawishi asilimia 18 ya wapiga kura ambao wagombeaji wao walishindwa.

Isabella Mwagodi