1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano Gaza yaendelea

18 Novemba 2012

Israel imeshambulia maeneo ya wapiganaji katika ukanda wa Gaza kwa siku ya tano Jumapili(18.11.2012),wakishambulia kwa ndege na jeshi la majini wakati jeshi lake likijitayarisha kufanya mashambulizi ya ardhini.

https://p.dw.com/p/16l84
An explosion and smoke are seen after Israeli strikes in Gaza City November 17, 2012. Israeli aircraft pounded Hamas government buildings in Gaza on Saturday, including the building housing the prime minister's office, after Israel's Cabinet authorised the mobilisation of up to 75,000 reservists, preparing the ground for a possible invasion into Gaza. REUTERS/Suhaib Salem (GAZA - Tags: CIVIL UNREST MILITARY POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Jengo la ofisi ya waziri mkuu Haniyah mjini Gaza limeshambuliwaPicha: Reuters

Misri hata hivyo inaona ishara za uwezekano wa kupatikana usitishaji wa mapigano hapo katika siku za baadaye.

Wapalestina 47, karibu nusu yao wakiwa ni raia, ikiwa ni pamoja na watoto 12, wameuwawa katika mashambulio hayo ya Israel , maafisa wa Palestina wamesema. Karibu maroketi 500 yaliyofyatuliwa kutoka Gaza yamefika nchini Israel, na kuuwa watu watatu na kuwajeruhi wengine kadha.

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service A general view of the Arab foreign ministers emergency meeting on the military operation in the Gaza Strip at the Arab League headquarters in Cairo November 17, 2012. Arab foreign ministers will consider on Saturday a draft statement that calls for the Arab League chief to lead a delegation to Gaza and voices support for Egypt's efforts to negotiate a truce, an Arab diplomatic source said. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Kiarabu mjini CairoPicha: Reuters

Israel ilianzisha mashambulizi yake makubwa ya anga siku ya Jumatano, na kumuua kiongozi mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas , kwa lengo la kuwazuwia wapiganaji katika eneo hilo la pwani kushambulia kwa maroketi jamii inayoishi katika eneo lake la kusini mwa nchi hiyo.

Makombora 950 yaanguka Gaza

Taifa hilo la Kiyahudi limeshambulia hadi sasa kwa makombora 950 kwa kutumia ndege za kijeshi dhidi ya eneo hilo dogo la pwani la Wapalestina, wakilenga vifaa vya kijeshi pamoja na kubomoa nyumba za wapiganaji na makao makuu.

Mashambulio yaliendelea usiku wa manane Jumapili, huku ndege za kivita zikishambulia maeneo kutoka baharini. Shambulio la anga lililenga katika jengo mjini Gaza ambalo ni la ofisi za chombo cha habari cha Kiarabu na kuwajeruhi waandishi watatu wa televisheni ya al Quds, kituo cha televisheni ambacho Israel inakiona kuwa kinaunga mkono kundi la Hamas, wamesema watu walioshuhudia.

Mashambulio mengine ya alfajiri dhidi ya nyumba katika kambi ya wakimbizi ya Jebalya yamesababisha kifo cha mtoto mmoja na kuwajeruhi watu wengine 12, wamesema maafisa wa hospitali.

epa03473593 Israeli couple and their son run for cover as a siren sounds in Tel Aviv on 16 November 2012. Two rockets were fired from Gaza towards Tel Aviv today and landed in an open area. today and yesterday is the first time after 21 years from the Gulf War that a real time siren sounds in Tel Aviv EPA/ABIR SULTAN
Watu wakikimbia kujisalimisha mjini Tel Aviv -Picha: picture-alliance/dpa

Mashambulio haya yanafuatia taarifa za kikaidi zilizotolewa na msemaji wa kijeshi wa Hamas Abu Ubaida, ambaye amesema katika mkutano na waandishi habari kuwa, "duru hii ya mapambano haitakuwa ya mwisho dhidi ya maadui wa kizayuni na ndio kwanza inaanza."

Majengo yaharibiwa

Shambulio la Israel siku ya Jumamosi limeharibu nyumba ya kamanda wa Hamas karibu na mpaka na Misri.

Israel hata hivyo ikiwa na vifaru na vifaa vingine vya kijeshi imeweka majeshi yake katika mpaka, ikiashiria kuwa bado inafikiria uwezekano wa mashambulio ya ardhini ndani ya Gaza.

A 155mm mobile cannon (front) is seen after it was transported to an area just outside the northern Gaza Strip November 15, 2012. Two rockets fired from the Gaza Strip targeted Tel Aviv on Thursday in the first attack on Israel's commercial capital in 20 years, raising the stakes in a showdown between Israel and the Palestinians that is moving towards all-out war. REUTERS/Amir Cohen (ISRAEL - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Majeshi ya Israel yakiwa tayari kwa shambulio la ardhini GazaPicha: Reuters

Baraza la mawaziri la Israel limeamua siku ya Ijumaa, (16.11.2012) kuongeza mara dufu idadi ya wanajeshi wa akiba katika operesheni ya Gaza kufikia 75,000 na wanajeshi wa akiba wanaofikia 16,000 tayari wamekwishaitwa.

Israel imesema kuwa shule katika eneo lake la kusini zitafugwa leo Jumapili(19.11.2012) kuepuka madhara zaidi kutokana na mashambulio ya maroketi ambayo yamefika hadi katika mji mkuu Tel Aviv katika siku chache zilizopita.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Grace Patricia Kabogo