1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano Gaza

16 Mei 2007

Mapigano baina ya makundi ya Hamas na Fatah yanaendelea eneo la Gaza huku watu kadha wakiripotiwa kuwawa na wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/CHEG

Mfalme wa Jordan Amezisihi pande zote zinazopigana maeneo ya wapalastina zikubali kuweka silaha zao chini kwa Maslahi ya wapalastina, na kwamba kuendelea kwa mapigano hayo kutawafaidisha wa Israel kuliko wapalastina .

Idadi ya watu waliofariki sasa imefikia watu 37 katika muda wa siku nne zilizopita

Kwa maelezo zaidi huyu hapa Omar Mutasa.

Akihojiwa na gazeti la Al-Arab Al-Yawm la mjini Amman nchini Jordan ,Mfalme Abdullah wa pili amesema, anasikitishwa na ugonvi wa ndani wa wapalastina huko ghaza, na mapigano hayo yakizidi kuendelea, Mfalme Abdullah amesema, huenda yakaathiri maendeleo ya mazungumzo ya Amani.

Wanamgambo wa kundi la Hamas leo wamewaua

Wafasi 6 wa kundi la Fatah licha ya kutolewa miito ya kusitisha mapigano hayo .

Kwa muda wa siku nne zilizopita watu 37 wameripotiwa kuwawa katika ukanda wa ghaza,

na wengi kujeruhiwa.

Mfalme Abdullah amesema Jordan na Misri nchi za kiarabu zilosaini mkataba wa Amani na Isreal, viongozi wa kiarabu wamezipendekeza nchi hizo kuishawishi Israel ikubali kuondoka katika maeneo ya waarabu ilio yateka tangu mwaka 67 na pia kuwaruhusu wakimbizi wakipalastina kurejea makwao,

ndipo waarabu watakua tayari kurejesha uhusiano kamili na Israel ,lakini Israel imelikata suala la kurejea makwao wakimbizi waki palastina .

Huu ni wakati muhimu katika historia ya wapalastina,na kuendelea kwa mapigano haya baina ya kundi la Hamas na Fatah, kunazidi kudidimiza matumaini ya wapalastina, na Israel, ndio inayofaidika amesema Mfalme Abdullah.

Siku tatu zilizopita Mfalme Abdullah wa Jordan alikutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert katika mji wa Aqaba ulioko bahari ya sham na Mfalme Abdullah sasa anapanga kukutana na Rais wa palastina ,Mahmoud Abbas(Abu mazen) katika kongamano la kiuchumi la kimataifa litakalo fanyika nchini Jordan ijuma ijayo, na amesema atajaribu kuwakutanisha viongozi hao wawili .

Viongozi wa palastina na Israel walikubaliana mwezi March wawe wakifanya mazungumzo ya mara kwa mara lakini hilo halikuezekana mwezi jana pale waziri mkuu wa Israel aliposhinikizwa kujiuuzulu kufatia vita vya mwaka jana dhidi ya Lebanon.

Wakati huo huo viongozi wa nchi 6 wanachama wa ushirikiano wa mataifa ya ghuba wametoa taarifa ya kuyalaani mapigano hayo ya wapalastina, na wamewataka viongozi wa Hamas na Fatah wauihishimu mkataba wa Maccah uliosimamiwa mwezi March na mfalme wa Saudi Arabia .

Nae waziri wa Habari wa palastina Mustafa Barghouti amesema, leo pamekueko mazungumzo kwa njia ya simu baina ya Rais Mahmoud Abbas wa palastina na kiongozi wa Hamas, Khaled Mishaal anaeishi uhamishoni nchini Syria.

Viongozi hao wamekubaliana kutafuta njia za kukomesha mapigano yanayoendelea eneo la ghaza.