1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano Mashariki mwa Kongo yazuka upya

16 Septemba 2008

Mapigano yamezuka upya Mashariki mwa Congo kati ya waasi wa kundi la CNDP la Generali Laurent Nkunda na majeshi ya serikali.

https://p.dw.com/p/FJEx
Rais Kabila wa DRC yuko katika ziara ya eneo la mapigano la Kivu ya KaskaziniPicha: AP

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yuko katika ziara ya eneo hilo la mapigano la Kivu ya Kaskazini na inaelezwa hadi sasa hakutoa taarifa yoyote ile hadharani juu ya ziara yake hiyo ambayo ni nadra kufanya katika eneo la mapigano.

Mohamed Dahman alipata fursa ya kuzungumza na mkaazi mmoja wa Goma mji mkuu wa Kivu ya Kaskazini Paterne Inga juu ya mapigano hayo.