1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano Srilanka

Mohammed AbdulRahman2 Desemba 2007

Mapigano Srilanka

https://p.dw.com/p/CVjV

Colombo:

Wanajeshi wa serikali ya Srilanka wanaendelea na hujuma zao dhidi ya waasi wa kundi la Tamil Tiger kaskazini mwa kisiwa hicho. Duru za kijeshi zimesema zaidi ya waasi 20 waliuwawa katika mapigano hayo. Wanajeshi kadhaa wa serikali waliuwawa au kujeruhiwa. Waasi wa Tamil Tiger , wamekua wakipigania uhuru wa eneo la kaskazini na mashariki mwa Srilanka tangu 1983. Zaidi ya watu 70,000 wameuwawa katika mgogoro huo.