1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapinduzi Mali yaitisha Niger

4 Mei 2012

Maafisa wa Niger taifa jirani na Mali ambalo limekumbwa na mapinduzi na kuligawa mara mbili, wameonya kuwa hali ya mapinduzi katika ukanda huo unaweza kuenea kwenye mataifa mengine kama tahadhari haitochukuliwa.

https://p.dw.com/p/14pOz
Mmojawapo wa wapiganaji nchini Mali
Mmojawapo wa wapiganaji nchini MaliPicha: Fatoumata Diabate

Mohammed Anacko ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa wanamgambo wa Tuareg katika nchi ya Niger anasema utulivu wa eneo hilo utategemea sana juhudi za Mali kulishughulikia tatizo hilo kwa kina. Kwa hakika idadi ya wakaazi wa Kaskazini mwa Mali na wakaazi wa Niger ni sawa na wako katika hatari moja.

Tahadhari hiyo inalingana na ya Waziri Mkuu wa taifa hilo Brigi Rafini aliyewataka Waniger kuepuka kuwa wahanga wa makundi yanayoleta mgawanyiko na kuwa wanajukumu la kulinda utamaduni wao na kulinda umoja wa taifa lao.

Historia ya Mapinduzi

Taifa hilo linatakiwa kustushwa na mapinduzi ya Mali kwani historia inabainisha kuwa Mali na Niger ni mataifa yenye udugu wa damu na ujirani wa karibu sana. Mara baada ya wanamgambo hao wa Tuareg kufurushwa Mali na kukimbilia Kaskazini ya Mali. Umbali wa kutoka Niamey kuelekea eneo la Watuareg wengi ni Kilometa 450 tu wakati umbali kutoka walipo Watuareg na mji Mkuu wa Mali Bamako ni mbali zaidi.

Mojawapo ya familia huko Maradi, Niger
Mojawapo ya familia huko Maradi, NigerPicha: DW

Wapigananji wa Tuareg ambao wameasi zaidi ya mara 5 tangu mwaka 1916 kwa madai ya umasikini wa eneo lao kwa muda mrefu na kudai pia kutengwa na serikali zao kuwa mbali nao kabisa. Wakiwa wanambinu mpya za kivita sasa wapiganaji hao wanaonekana kuwa na silaha zenye ubora zaidi na magari ya kivita wakifanya uharibifu kupitia jangwa sahara wakitokea Libya.

Mojawapo ya tukio kubwa la mapinduzi hivi karibuni limefanywa na wapigananaji wa Tuareg wa Mali, MNLA ambapo walijitangazia mamlaka katika eneo kubwa la jangwa na kuliita taifa jipya la Azawad, ikiwa ni baada ya mapigano ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu na wanamiliki theluthi mbili ya eneo zima la Mali.

Utajiri wa Niger

Kuwaacha wapiganaji hao kuingia Niger ni hatari kwani kunaweza kuibua wakimbizi na kukumbwa na uhaba wa chakula mara baada ya ujio huo. Pia kunaweza kuzuia uwekezaji katika taifa hilo kwani Niger ina utajiri mkubwa wa madini ya uranium ambapo kuna mradi unaoendeshwa na Kampuni ya Areva ya Wafaransa na Wachina.

Eneo hilo lenye jangwa kubwa ni kivutio kikubwa cha watalia kutoka Ulaya ambao walikuwa wakifika kuona hali ya jangwa ilivyo cha kusikitisha mara baada ya wapiganaji hao kuibuka na harakati zao mwaka 2007 na 2009 na kuongezeka mauaji kadhaa sasa hakuna kabisa watalii katika eneo hilo ambapo wapiganaji hao wanahusishwa na ushirikiano na al-Qaeda.

Ushiriki wa vijana kwenye uhalifu

Saadick Idrissa ambaye ni mtumishi wa shirika moja lisilo la kiserikali anasema kukiwa na uhaba wa ajira, vijana wengi toka eneo hilo sasa wanajiingiza katika ujambazi, ukabaji na kujiunga kwenye makundi mengi ya kialifu. Sasa wao wameamua kujikita kuwaelimisha ili kujishughulisha na shughuli za maendeleo badala ya uhalifu.

Hali hii inathibitishwa na Karim al Kassoum mwenye umri wa miaka 22 anasema atafanya kazi yoyote ile atakayopewa kama kwenda Mali au akimaanisha kushiriki mapigano.

Wakaazi wa eneo hili hawana matumaini kabisa na serikali yao kwani tatizo la umasikini na uhaba wa ajira bado ni sekeseke kubwa.

Mohamed Yacoubou kutoka Tchintabareden anasema viongozi wao hawawezi kufanya lolote la maana bali wakichanguliwa tu wanaenda kukaa Niamey kwenye majumba yenye viyoyozi.

Wanajeshi wa Mali wakizunguka mitaani mjini Bamako baada ya machafuko
Wanajeshi wa Mali wakizunguka mitaani mjini Bamako baada ya machafukoPicha: Reuters

Lakini Niger inatazamwa imejitahidi mno kuwakabili wapiganaji waliokuwa wakimuunga mkono Hayati Muammar Gaddafi lakini imekuwa kinyume kwa Mali ambayo sasa inakumbwa na mgogoro huo wa mapinduzi ya hapa na pale.

Maafisa wa Niger wanaongeza kuwa kwa kiwango kikubwa taifa lao limeweza kuwadhibiti wapiganaji hao lakini kumekuwa hakuna tatizo la kikabila kama llivyo Mali. Alkache Akhada ambaye ni Mtuareg na Kaimu Mkurugenzi wa baraza lao anasema kwa hakika kila kona ya Niger kuna Watuareg ambapo kwa nchi ya Mali hakuna mseto kama wao.

Kutokana na hali kuwa ya mashaka Nchini Mali Jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi-ECOWAS imepanga kupeleka kikosi cha wanajeshi 3000 kusaidia kuirudisha nchi hiyo katika amani na utawala wa kidemokrasi haraka iwezekanavyo.

Mwandishi:Adeladius Makwega

Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman