1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko ya ardhi yaua watu 80.

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgZj

Java , Indonesia. Maporomoko ya matope katika eneo la kati la jimbo la Java nchini Indonesia limesababisha karibu watu 80 kuuwawa ama hawajulikani waliko. Huduma za uokozi zimesema kuwa kiasi cha watu 61 wameuwawa katika tukio moja la maporomoko katika wilaya ya Karanganyar. Mamia ya wanajeshi,polisi na watu wa kujitolea wamekuwa wakijaribu kupata vifaa vizito vya kunyanyulia kwenda katika vijiji vilivyoathirika katika kisiwa kikubwa cha Java. Juhudi za uokozi zimezuiwa na barabara zilizojaa matope yaliyoporomoka pamoja na mafuriko. Maelfu ya watu wamepelekwa katika maeneo mengine baada ya nyumba zao kufunikwa na matope ama kuvunjwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha. Maafisa wa maeneo hayo wamesema maporomoko hayo ya milima ni mabaya kabisa kuwahi kutokea katika kisiwa cha Java katika muda wa miongo miwili.