1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko yahofiwa kuua watu zaidi 350 Uganda

2 Machi 2010

Wilaya ya Bududa nchini Uganda yakumbwa na maafa makaubwa

https://p.dw.com/p/MHsg
Baadhi ya maeneo ya milimani nchini UgandaPicha: DW/ Barbara Gruber

Nchini Uganda watu 45 wamefariki kufuatia maporomoko ya matope yaliyotokea wilayani Bududa, mashariki mwa Uganda.

Kiasi cha watu wengine 350 wanahofiwa kuwa wamezikwa na matope hayo yaliosababishwa na mvua nyingi zilizoanza kunyesha kiasi cha wiki mbili zilizopita.

Eneo hilo la mkasa liko karibu na mlima wa Elgon ulio kwenye mpaka na nchi ya Kenya. Baadhi ya sehemu za Uganda na Kenya zimepata mvua nyingi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita wakati ambapo ni msimu mkavu, kwa kawaida.

Sikiliza taarifa ya Leyla Ndinda kutoka Uganda