1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO: Mvua kubwa zasababisha mafuriko kusini mwa Afrika

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCU0
Rais Jemadari Pervez Musharraf akitangaza amri ya hali ya hatari tarehe 3 Novemba mjini Islamabad
Rais Jemadari Pervez Musharraf akitangaza amri ya hali ya hatari tarehe 3 Novemba mjini IslamabadPicha: AP

Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa majuma manne nchini Msumbiji,serikali imewataka wakazi katika maeneo yanayokabiliwa na hatari ya mafuriko,waondoke sehemu hizo.Waziri mkuu Luisa Diogo amesema,mafuriko hayo huenda yakawa mabaya zaidi kuliko yale yaliotokea miaka saba ya nyuma.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Afrika ya Kusini, sehemu zilizoathirika ni maeneo ya kati ya Msumbiji yalio ukingoni mwa Mto Zambesi pamoja na mito mingine midogo iliyo karibu.Mvua kubwa zilizonyesha,zimeathiri pia nchi za jirani Zambia,Malawi na Angola.