1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maputo.Samora Machel akumbukwa nchini Msumbiji.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1E

Rais wa Msumbiji Armando Guebuza amezindua sherehe za miaka ishirini tangu kufariki kwa shujaa wa Uhuru Samora Machel aliyefariki katika ajali ya ndege.

Guebuza aliyeweka jiwe la msingi la kumbu kumbu ya Machel katikati ya mji mkuu Maputo amesema, uamuzi wa kuanzisha siku hii ni kuonyesha jitihada alizozifanya Samora Machel katika wakati wa uhai wake kwa wananchi wa Msumbiji.

Rais Guebuza na Rais wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki hii leo walitarajiwa kulitembelea eneo lililotokea ajali huko Afrika ya Kusini, karibu na mpaka wa Msumbiji.

Samora Machel aliyeisaidia Msumbiji kupata uhuru kutoka kwa Wareno, na kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo, alikufa kwa ajali ya ndege akiwa na watu wengine 34, katika eneo la Mbuzini Kaskazini mwa Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1986.