1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marafiki wa Syria wakutana mjini Tunis

24 Februari 2012

Baada ya maaazimio kadhaa ya Umoja wa Mataifa kushindwa kuleta suluhisho nchini Syria, jumuiya ya kimataifa sasa inatafakari njia nyingine za kuushinikiza utawala wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/149Ni
Marafiki wa Syria wakutana mjini TunisPicha: AP

Kwenye mkutano wao katika mji mkuu wa Tunsia, Tunis wajumbe kutoka nchi 70 pamoja na mashirika ya kimataifa pia watazitathmini jumuiya za wanaharakati wa upinzani. Lakini swali kubwa ni jumuiya gani?

Mtaalamu wa masuala ya Syria kwa muda wa miaka mingi, Robert Fisk anaeleza matatizo yanayowakabili wapinzani. Wakati wote wanapokutana na wawakilishi wa serikali za nje, viongozi wa wanaharakati wa upinzani wanaambiwa, tafadhali zungumzeni kwa sauti moja .

Lakini hawafanyi hivyo." Mtaalamu mwengine Taufiq Rahim anatueleza sababu za mikanganyiko miongoni mwa wanaharakati wa Syria.

Kuna baraza la kitaifa la Syria,kamati za uratibu za kitaifa na za majimbo,pia lipo jeshi huru la askari waliolikimbia jeshi la serikali na vipo vikosi mchuruziko.

Assad kwa sasa bado anao wafuasi asilimia 20. Wangelikuwa wachache zaidi iwapo wapinzani wangelisimama pamoja na iwapo wangelikijua wanachokitaka."

Wapinzani waliopo nje na wapinzani wa ndani, wale wanaoendesha kampeni ya amani na wale wanaopambana kwa silaha- hao wote hawana mwongozo mmoja. Aghalabu hawajuani na kwa hivyo hawaaminiani. Hilo ndilo tatizo linalowakabili marafiki wa Syria wanaokutana mjini Tunis. Wanataka kuyatathmini makundi ya wapinzani nchini Syria.

Kundi linalostahili kuungwa mkono

Nchi za mstari wa mbele miongoni mwa marafiki wa Syria ni Marekani,Ufaransa,Uingereza na Ujerumani kama ilivyo kwenye Umoja wa Mataifa-nchi hizo ndizo zinazoongoza njia katika kampeni inayoendeshwa katika nchi za magharibi dhidi ya utawala wa Assad.

Katika Mashariki ya kati bango limebebwa na Saudi Arabia na Katar. Lakini marafiki hao pia wamegawanyika juu hatua za kuchukua dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Hatua za kuchukua zinapaswa kuenda umbali gani gani? Urusi, kama ambavyo imetarajiwa, inataka serikali ya Syria ishirikishwe. Wanaharakati wa upinzani waliomo katika Baraza la Kitaifa wanaoishi nje ndiyo wanaopendelewa duniani-

Lakini kwa wananchi wengi wa Syria waliopo nchini, wapinzani wanaoishi nje wapo mbali na nyumbani. Mwananchi mmoja Abdu Ahmad amesema upinzani wa amani ni upuuzi mtupu! Watu wengi nchini Syria wanao mtazamo huo. Wanaliunga mkono jeshi huru la waasi.

Upinzani wa amani dhidi ya utawala wa Assad hauna mashiko kwa mtazamo wa watu wengi nchini Syria, na hasa baada ya Urusi na China kutumia kura za turufu kulipinga azimio juu ya Syria hivi karibu, kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

United Nations Secretary General Kofi Annan speaks in front of journalists during his last official press conference at the United Nations European headquarters in Geneva, Switzerland, Tuesday, November 21, 2006. Kofi Annan will leave his post of United Nations Secretary General at the end of the year. (KEYSTONE/Salvatore Di Nolfi)
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi AnnanPicha: AP

Annan ateuliwa mjumbe maalum

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa Syria, kabla ya kuanza kwa mkutano wa "Marafiki" wa Syria mjini Tunis utakaojadili mgogoro wa nchi hiyo.

Bwana Annan ameteuliwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu.

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu wamesema jukumu la Bwana Annan litakuwa kukomesha mauaji na kukiukwa haki za binadamu na kuhimiza juhudi za kuleta suluhisho la amani.

Uteuzi wa Annan ulifanyika kabla ya mazungumzo ya mjini London ambako, kwa mujibu wa taarifa, Marekani, Ulaya na nchi za Kiarabu zilitayarisha onyo kali kwa Rais Assad, la kumtaka akubali kusimamisha mashambulio mara moja au atawekewa vikwazo madhubuti.

Mwandishi/Leidholdt,Ulrich/

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mhariri/ Josephat Charo