1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani haina uhakika kama mashambulizi ya Libya yalipangwa

15 Septemba 2012

Marekani imesema kuwa hakuna taarifa zilizopatikana hadi sasa zinazoonyesha kuwa mashambulizi yaliyofanyika kwenye ubalozi wa nchini hiyo mjini Benghazi nchini Libya yalipangwa.

https://p.dw.com/p/169aG
Tunisian police stand by during a demonstration in front of the U.S. embassy in Tunis September 14, 2012. At least five protesters were wounded when Tunisian police opened fire on Friday to quell an assault on the U.S. embassy compound in the capital Tunis, a Reuters reporter said. It was not immediately clear if police fired live rounds or rubber bullets. A large fire erupted inside the compound which has been invaded by hundreds of people incensed by a U.S.-made film that demeans the Prophet Mohammad. REUTERS/Zoubeir Souissi (TUNISIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CRIME LAW RELIGION)
Protest Mohammed Film Anti Islam Tunesien TunisPicha: Reuters

Taarifa hiyo inakuja wakati miili ya watu wanne waliouawa kwenye mashambulizi dhidi ya ubalozi huo ikiwa imeshawasili nchini Marekani.

Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa taifa hilo halitasahau kujitolea kwa watu hao. Obama alimsifu Balozi Christopher Stevens, mwanadiplomaisa Sean Smith na maafisa usalama Tyrone Woods pamoja na mwenziwe Glen Doherty kwa kujitolea maisha yao kwa ajili ya wengine na kusema kuwa kazi yao itaendelezwa.

"Marekani haitasalimu amri kwa dunia. Hatutaacha kufanya kazi kwa ajili ya uhuru na utu ambao kila mtu anastahiki kuupata" alisema Obama.

Maandamano ya kupinga filamu inayomdhalilisha Mtume Mohammad
Maandamano ya kupinga filamu inayomdhalilisha Mtume MohammadPicha: Reuters

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carne alisisitiza hapo kabla kwamba tukio la kushambuliwa kwa ubalozi huo bado liko chini ya upepelezi. " Hatuna taarifa zinazoonyesha kwamba yalikuwa ni mashambulizi ya kupangwa" aliwaambia waandishi wa habari.

''Ghasia tunazoziona katika nchi mbalimbali za ulimwengu wa kiarabu zinatokana na mkanda wa video ambao waislamu wengi wanauona kuwa umewadhalilisha. Wakati machafuko yanayoendelea yakiwa hayana utetezi, tunasema kuwa filamu hiyo si majibu ya tukio la kumbukumbuku ya mashambulizi ya Septemba 11", aliongeza Carne.

Kuimarishwa usalama Libya

Uongozi wa Libya na maafisa wa Marekani hapo kabla walisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa yamepangwa. Uongozi nchini humo ulisitisha safari zote za ndege Benghazi ambao ni mji wa bandari ulioko mashariki mwa nchi hiyo na wa pili kwa ukubwa. Hata hivyo afisa wa serikali mjini humo amesema kuwa shughuli hizo zimefunguliwa tena na ndege za ndani na nje zitaanza kuruka tena.

Maandamano ya Sudan kupinga filamu
Maandamano ya Sudan kupinga filamuPicha: Reuters

Naibu waziri wa usafiri Fawzi Beltamr amekiambia kituo cha televisheni cha taifa kuwa huduma hiyo imerejea baada ya kuhakikisha kuwa eneo hilo la uwanja wa ndege liko salama. Amesema huduma zilifungwa jana (14.9.2012) kutokana na milio ya risasi iliyokuwa inasikika karibu na eneo hilo.

Washukiwa baadhi wakamatwa

Tayari watuhumiwa kadhaa wamekamatwa kuhusiana na mauwaji ya Jumatano kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani Wanis al-Sharif ambaye alikataa kutoa taarifa zaidi. Wapelelezi wa Libya walikuwa wanafuatalia uvumi kuwa mashambulizi hayo yalipangwa kama sehemu ya kumbukumbu ya mashambulizi ya Septemba 11 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2001.

Hata hivyo bwana Carney amesema kuwa ni mapema mno kutoa jibu kamili kuhusu mashambulizi hayo. Amesema kuwa kwa sasa Marekani inaelekeza nguvu zake kwenye kuzilinda balozi zake ambazo maelfu ya waandamanaji katika nchi za kiarabu wamekuwa wakizivamia kupinga filamu inayomkashifu Mtume Muhammad iliyotengenezwa nchini humo.

Maandamano India kupinga filamu
Maandamano India kupinga filamuPicha: dapd

"Tunafanya kazi na serikali mbalimbali kwenye nchi ambazo zina maandamano, kuzikumbusha juu ya wajibu wao wa kutoa ulizi wa uhakika kwa wafanyakazi wa balozi na mali kwenye ofisi hizo. Tunawahakikishia kuwa vifaa na rasilmali za kutosha zimewekwa kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kulinda usalama.

Rais Obama ametuma barua kwa Baraza la Congress la Marekani kuliambia kuwa ametuma vikosi vya kijeshi kusaidia kuwalinda wafanyakazi wa balozi za nchi hiyo walioko Libya. Mashambulizi hayo yamefanyika katikati ya maandamano ya watu wenye hasira wanaopinga kudhalilishwa kwa mtume wao.

Mwandishi: Stumai George/dpa

Mhariri: Daniel Gakuba