1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Marekani imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 100 kwa Haiti

Sudi Mnette
23 Septemba 2023

Serikali ya Marekani imeahidi kutoa dola milioni 100 kwa shabaha ya kuunga mkono juhudi ya kuundwa kikosi cha kimataifa kitakachongozwa na Kenya katika kurejesha usalama nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4Wixz
UNO Haiti | Vollversammlung | Ariel Henry
Picha: Craig Ruttle/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Marekani imeahidi kutoa dola milioni 100 kwa shabaha ya kuunga mkono juhudi ya kuundwa kikosi cha kimataifa kitakachongozwa na Kenya katika kurejesha usalama nchini Haiti, taifa la visiwa vya Karibiani lililokumbwa na mizozo.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kuwa taifa lake litatekeleza wajibu huo kwa  kutoa vifaa, ikiwa ni pamoja na mafunzo, ndege, nyenzo za mawasiliano na usaidizi wa matibabu, baada ya kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amesifu hatua hiyo akisema polisi na wanajeshi wanahitajika, na kwamba utumiaji wa nguvu ndio njia pekee itakayosadia kuandaa mazingira kwa serikali kutekeleza majukumu yake tena.Mbali na Kenya, mataifa mengine ambayo yametoa ahadi ya kupeleka vikosi Haiti ni Jamaica, Bahamas, na Antigua na Barbuda.