1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani ina wasiwasi kuhusu kuzuiliwa wapinzani Urusi

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CT37

Marekani imeeleza wasiwasi wake kuhusu jinsi maafisa wa polisi nchini Urusi walivyoyashughulikia maandamano ya kuipinga serikali na kukamatwa na kuzuiliwa kwa Garry Kasparov pamoja na viongozi wengine wa upinzani.

Kasparov amehukukumiwa kifungo cha siku tano jela kwa kuongoza maandamano dhidi ya rais Vladamir Putin, juma moja kabla uchaguzi wa bunge kufanyika nchini Urusi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, Sean McCormack, amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa kuhusu kukamatwa na kuzuiliwa kwa viongozi wa upinzani na ametoa mwito waruhusiwe kuwa na mawakili na watendewe haki.

Tangazo la Marekani limetolewa wakati Urusi ikimzuilia kiongozi mwingine wa upinzani, Boris Nemtsov, na wengine takriban 200 waliokamatwa wakati wa maandamano ya jana mjini St Petersburg.