1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuanzisha mpango maalum kwa Afrika

1 Februari 2007

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon inatarajiwa kuanzisha kitengo maalum cha ulinzi.

https://p.dw.com/p/CHKv
Rais George W Bush wa Marekani
Rais George W Bush wa MarekaniPicha: AP

Mpango utakaojulikana kama AFRICOM unatazamiwa kutangazwa rasmi na rais George W Bush wa Marekani wiki ijayo wakati ambapo kiongozi huyo atawasilisha mswaada wa bajeti ya mwaka 2008 mbele ya Kongress.

Taarifa hiyo inathibitisha kuwa bara la Afrika linakabiliwa na vitisho na kwa hivyo linahitaji kutazamwa kwa karibu zaidi na Pentagon kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Swala jingine la muhimu kabisa ni kuhusu mchango wa Afrika katika vita vya kupambana na ugaidi ama kama Pentagon inavyo viita vita vya muda mrefu pia mswaada huo wa rais Bush unaangalia mali asili za Afrika hasa mafuta na gesi katika uchumi wa dunia na wakati huo huo ushindani na China miongoni mwa nchi zingine zinazo shindania mali asili za bara la Afrika.

Kuanzishwa kwa kitengo cha AFRICOM kunaungwa mkono na vyama vyote katika bunge la Kongress.

Kuwepo kwa jeshi la Marekani katika eneo la upembe wa Afrika na sehemu za maeneo yenye utajiri wa mafuta na gesi huko Afrika Magharibi kumeongezeka hasa baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 tukio ambalo lilisababisha utawala wa rais Bush kuanzisha vita dhidi ya ugaidi duniani kote.

Seneta wa chama cha Demokratik Russell Feingold ambae pia ni mwenyekiti wa maswala ya Afrika amesema kitengo hicho maalum cha jeshi la Marekani ni cha muhimu sana kwa usalama wa taifa hilo.

Pia amesisitiza kuwa kitengo hicho kitawezesha kuwepo uhusiano wa karibu na bara la Afrika na wakati huo huo kuzilinda nchi hizo zisitumiwe na maadui dhidi ya Marekani na washirika wake.

Kutoka mwaka 2002 jeshi la Marekani lilikuwa limewekeza nguvu zake katika nchi ya Djibouti ambako kuna takriban wanajeshi 1900 wa kimarekani.

Watalaamu wa Afrika pia wanaunga mkono wazo la kuanzishwa kitengo maalumu cha Pentagon katika nchi za Afrika wanasema kuwa iwapo nia na madhumuni yataambatana sambamba na mipango mingine kwa Afrika kama vile kuungwa mkono umoja wa nchi za Afrika na kuwezesha shughuli za kulinda amani vyote hivi vikiwekwa chini ya mwamvuli mmoja basi mswaada huo uatakuwa ni wenye mafanikio makubwa.

Jeniffer Cooke mtalaamu wa maswala ya kimataifa nchini Marekani anasema hatua hii itasaidia kuzielewa shida zinazo ikabili Afrika.

Lakini wakati huo huo wasiwasi hauachi kujitokeza kufuatia mswaada huo wa rais Bush wa kuanzishwa kitengo cha Pentagon katika bara la Afrika kwamba sharti lazima awepo muwakilishi wa cheo cha juu wa serikali ya Marekani atakae hakikisha sera za nchi yake zinatimizwa.