1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kufuatilia kesi za viongozi wateule wa Kenya

2 Aprili 2013

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Marekani itafuatilia kwa makini hatua za viongozi wateule wa Kenya katika kukidhi matakwa ya mahakama ya uhalifu ya kimataifa -ICC- kutokana na tuhuma zinazowakabili.

https://p.dw.com/p/1882B
Mahakama ya ICC mjini The Hague
Mahakama ya ICC mjini The HaguePicha: Getty Images

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari msemaji wa wizara hiyo Hilary Renner amesema watashiriki ipasavyo katika kulifuatilia suala hilo. Kutokana na kauli hiyo Sudi Mnette amezungumza na Geofrey Musila, mwanasheria wa kimataifa na mchambuzi wa siasa za Kenya, aliyejikita hasa katika masuala ya ICC na kwanza anaelezea kwanini marekani imeibuka na suala hili wakati huu. Kuskiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman