1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani mwanachama Tume ya Haki za binadamu

13 Mei 2009

Kwa mara ya kwanza Marekani imechagua kujiunga na Tume hiyo.

https://p.dw.com/p/Hp7Z
( Barack Obama -kulia)Picha: AP

Marekani ,imechaguliwa katika Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na hivyo, yatazamiwa kutoa mchango mkubwa katika shughuli za Baraza hilo la Kimataifa.Sera za nje za Marekani chini ya uongozi wa Rais Barack Obama, zimejitokeza tena katika uanachama huo kwenye Baraza hilo linalotetea haki za binadamu.Kwani, kwa wingi mkubwa,Marekani imechaguliwa kujiunga na Halmashauri hiyo.Kwa mara ya kwanza Marekani inajiunga na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.Baraza kuu la UM jana liliichagua Marekani kujiunga na Baraza hilo tena kwa wingi mkubwa wa hadi 90%.

"Nchi zinazoungamkono uanachama wa marekani ni 167.Ninatoa pongezi kwa zile nchi zilizochaguliwa kuwa wanachama wa baraza la Haki za Binadamu la UM."

Alitangaza jana Mwenyekiti wa Baraza hilo. Kwa hatua hiyo, Marekani imeachana na tabia yake ya kulisusia Baraza hilo lililoasisiwa miaka 3 nyuma.hii ni dalili la mabadiliklo ya msimamo anauchukua rais Obama katika sera za kimataifa kinyume kabisa na mtangulizi wake george Bush.Kuungwamkono kwa sauti nyingi uanachama wa Marekani, kunabainiha,kwamba walimwengu nao wamekukaribisha.Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa mataifa Bibi Susan Rice akasema:

"Tunaonesha shukurani zetu kuwa, Marekani imeshajiishwa kutoa mchango mkubwa pia katika UM katika swali muhimu kama vile haki za binadamu na demokrasia."Alisema bibi Susan Rice. Miongoni mwa nchi nyengine zilizochaguliwa kujiunga na baraza hilo ni China, Urusi,Kuba na hata saudi Arabia . Vikundi vya wakereketwa wa haki za binadamu vimekosoa mno hatua hiyo, kwani vimedai nchi hizo haziheshimu haki za binadamu na kuwa kama hapo kabla haki za binadamu nchini mwao zinakanyagwa kwa mguu.

Akijibu ila hizo zilizotolewa, mjumbe wa Marekani Bibi Rice alisema:

"Bila shaka daima kuna nchi ambazo rekodi zao za kuheshimu haki za binadamu si nzuri kabisa.Na sisi binafsi timekuwa na kasoro zetu."

Ujerumani baada ya kuwa mwanachama kwa miaka 3 wa Baraza hilo sasa si mwanachama tena.Baraza la Haki za Binadamu la UM hukutana mjini Geneva na lina wanachama 47 na 18 kati yao walichaguliwa upya hapo jana .Jukumu lake ni kulinda haki za binadamu katika nchi zanachama za Umoja wa Mataifa, likichukua nafasi ya Tume ya zamani ya Haki za Binadamu.(UN Human rights Commission).

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Muhammed Abdul-Rahman