1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Iran zaingia kwenye mvutano mpya

8 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cljv

WASHINGTON

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amesema Iran inajiingiza katika vitendo vya uchokozi dhidi ya Marekani kufuatia kisa cha wairan kutishia kuwaripua wanajeshi wa Marekani mwishoni mwa juma.Wanajeshi wa ulinzi wa Iran waliokuwa kwenye viboti vitano walitishia kuziripua meli tatu za wanamaji wa Marekani zilizokuwa zikifanya shughuli zake katika eneo la kimataifa la bahari ya ghuba ya Uajemi.Wanamaji hao wa Marekani walikuwa wameshajitaarisha kufanya mashambulizi lakini jeshi la Iran likageuza viboti vyake na kuondoka eneo hilo la hatari.Serikali ya Iran lakini haijalipa uzito suala hilo ikisema ni mambo ya kawaida yanayotokea mara kwa mara. Marekani lakini inadai huo ulikuwa uchokozi na waziri wake wa ulinzi Robert Gates amesema kitendo cha Iran kimewatia wasiwasi mkubwa na Marekani itakuwa tayari kupambana na hali yoyote ya uchokozi wa Iran dhidi ya wanajeshi wake au washirika wake.