1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Saudi Arabia zashtumu kurejea kwa vita Sudan

Tatu Karema
12 Juni 2023

Marekani na Saudia Arabia zimeshutumu vikali kuanzishwa tena kwa ghasia nchini Sudan baada ya muda wa kusitishwa kwa mapigano kwa saa 24 kati ya pande zinazozozana kumalizika.

https://p.dw.com/p/4SST9
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: Mohamed Nureldin Abdallah/REUTERS

Katika taarifa ya pamoja, Marekani na Saudi Arabia zilisema Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) waliweza kudhibiti vikosi vyao wakati wa muda huo lakini mataifa hayo mawili yamesononeshwa sana na hali ya kuanza kwa vurugu kali mara moja. Mapigano makali yameikumba Sudan tangu katikati ya Aprili, baada ya mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, anayeongoza kikosi cha RSF, kuanza kuzozana.