1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na uchaguzi wa kesho nchini Urusi

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVPN

WASHINGTON.Marekani imesema kuwa ina wasi wasi kuwa uchaguzi wa bunge nchini Urusi kesho Jumapili hautakuwa huru na haki na kwamba inaufuatilia kwa karibu.

Msemaji wa Rais Bush Dana Pperino amesema kuwa wana wasi wasi kuwa wananchi wa Urusi hawatapata nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa uhuru na haki.

Mapema wiki hii Rais Bush alielezea kusikitishwa kwake na kutiwa ndani kwa waandishi wa habari na wapinzani wa Rais Putin kuelekea kwenye uchaguzi huo na kutoa wito wa kuachiwa kwao.

Kampeni za uchaguzi wa bunge la nchi hiyo Duma, zilimalizika jana huku chama cha Rais Vladmir Putin cha United Russia Party kikitarajiwa kupata ushindi mkubwa.

Wakati huo huo Uhispania ambayo ni rais wa taasisi ya usalama na ushirikiano barani Ulaya imeitaka Urusi kufikiria upya uamuzi wake wa kujitoa katika mkataba wa kupunguza majeshi barani Ulaya.

Rais Vladmir Putin alitia saini sheria kuidhinisha kujitoa kwa Urusi katika mkataba huo ambao ulitiwa saini mwaka 1990 unaodhibiti uwekwaji wa silaha nzito barani ulaya.

Urusi inasema kuwa hatua hiyo ni kupinga mipango ya Marekani ya kutaka kuweka makombora ya kujihami katika nchi za Poand na Jamuhuri ya Czech