1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani. Obama anaongoza.

8 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cmbc

New Hampshire, Seneta Barack Obama amepata kura saba katika kura kumi zilizopigwa leo katika kitongoji cha Dixville Notch kwa upande wa chama cha Democratic katika jimbo la New Hampshire, wakati seneta John McCain ameshinda kwa upande wa chama cha Republican. Kura zilizopigwa na wapigakura wote 17 waliojiandikisha kupiga kura zilihesabiwa usiku leo Jumanne katika mji wa kando ulioko milimani ambapo sheria inahitaji kuwa vituo vya kupigia kura vifungwe mara uchaguzi unapokamilika na kutangazwa matokeo. Mbali ya zile za Obama kutoka jimbo la Illinois, seneta wa zamani wa jimbo la Carolina John Edwards amepata kura mbili na gavana wa New Mexico Bill Richardson amepata kura moja. Seneta wa jimbo la New York Hillary Clinton hakupata kitu.

Uchaguzi hata hivyo unaendelea katika maeneo mengine ya jimbo hilo la New Hampshire ambapo watu wengi wanatarajiwa kujitokeza. Huu ni uchaguzi uliowazi zaidi kwa Marekani katika muda zaidi ya miaka 50, ambapo rais aliyeko madarakani ama makamu wake hawawanii kuteuliwa.