1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani. Wananchi katika jimbo Hampshire wapigakura leo.

8 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CmRg

New Hampshire,

Wakaazi wa jimbo la New Hampshire nchini Marekani wanapiga kura katika hatua ya mwanzo ya uteuzi wa mgombea wa urais. Kura ya maoni inaonyesha kuwa Barack Obama wa chama cha Democratic anaongoza kwa asilimia kumi dhidi ya Hillary Clinton ambaye alikuwa hapo kabla akiongoza. Obama alimshinda Clinton wiki iliyopita katika uchaguzi wa jimbo la Iowa. Katika uchaguzi wa chama cha Republican katika jimbo hilo , kura ya maoni inamuweka John McCain mbele ya Mitt Romney. Watu wengi wanatarajiwa kujitokeza katika uchaguzi huo wa Hampshire. Huu ni uchaguzi uliowazi kabisa kwa Marekani katika kiti cha urais katika muda wa miaka zaidi ya 50, ambapo rais aliyeko madarakani ama makamu wa rais hawawanii kuteuliwa .