1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaanza kumtupaMusharraf ?

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlq

ISLAMABAD:

Marekani yabainika kuelemea sasa zaidi kwa tawi la wastani la viongozi wa jeshi la Pakistan pamoja na vikundi vya siasa wastani dhidi ya Jamadari Pervez Musharraf.Marekani inachukua msimamo huo katika juhudi za kutompoteza mshirika wake mkubwa katika vita dhidi ya ugaidi.

Wachambuzi wamegundua kwamba mnamo siku chache zilizopita,sera ya marekani imeanza kumuachamkono jamadari Musharraf na dhana hii imeimarishwa na ziara YA SASA YA MAKAMO WAKE WA WAZIRI WA NJE John Negroponte.

Negroponte akiwa nchini Pakistan, amemtaka rais wa Jamadari Musharraf kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa,kuondoa vizuwizi juu ya vyombo vya habari kuifuta hali ya hatari na kuhakikisha uchaguzi huru na bila mizengwe Januari,mwakani.Alisema,

Waziri huyo wa Marekani alizungumza pia kwa simu na kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto.

Hadi sasa , jamadari musharraf amekataa kuiondoa hali ya hatari aliotangaza akidai itaondoshwa tu pale hali ya usalama itakapotengenea.

Serikali yake imejaribu kuvifunga vituo 2 vikuu vya TV vya kibinafsi-GEO na ARYONE vilivyokuwa vikitangaza kutoka Dubai. Waandishi habari wa pakistan wamelalam ika juu ya ukaguzi wa habari kwa kuandamana katika mji wa Karachi.

Kutoka Washington,kuna taarifa kwamba Marekani inazingatia kumuacha mkono jamadari Musharraf.