1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaimarisha ulinzi

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8M

BERLIN:

Serikali ya ujerumani imearifu leo hatua za kuimarisha ulinzi katika taasisi na konsulati za kimarekani nchini Ujerumani kunafungamana na mipango ya waislamu wenye itikadi kali.

Kwa muujibu wa toleo la leo la jarida la Der Spiegel,kikundi cha wairaki wenye siasa kali Ansar al sunna,kinapanga hujuma dhidi ya Wamarekani na zana za Marekani ziliopo Ujerumani.

Ubalozi wa Ujerumani jana ulisema unaimarisha ulinzi kama jibu la hali ya wasi wasi .