1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yakiri Iran ilisitisha harakati za kutengeza bomu la nuklia 2003.

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWU9

WASHINGTON.Marekani imesema kuwa, shirika lake la ujasusi limebaini ya kwamba Iran ilisitisha harakati zake za kutengeneza bomu la nuklia mwaka 2003.

Hata hivyo shirika hilo limesema kuwa bado kuna tishio la nchi hiyo kuendelea na mpango wake huo kwani inaendelea na urutubishaji wa nishati ya uranium ambayo hutumika kutengeza bomu la nuklia.Iran imekuwa ikisisitiza kuwa nishati hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya kiraia.

Mshauri maalum wa Rais Bush katika masuala ya usalama Stephen Hadley amesema kuwa taarifa hizo za idara ya ujasusi ni mafanikio ya siasa za Rais Bush katika suala la Iran.

Iran kwa sasa inakabiliwa na vikwazo kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani kutokana na kukaidi azimio la kuitaka iache urutubishaji wa uranium.