1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yakosolewa na Jamadari Cross

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTG

LONDON:

Jamadari mwengine aliestaafu wa jeshi la uingereza amekosoa mkatati unaofuatwa na Marekani nchini Iraq.

Katika mazungumzo na gazeti la kila wiki litokalo jumapili-SUNDAY MIRROR-Meja-jamadri Tim cross ameieleza siasa ya Marekani nchini Irak imekwenda kombo mno.

„Yafaa kuamngaliwa hali hii kwa jicho la kile ilichoifika Marekani miaka ya karibuni katika vita vya Vietnam,hujuma kali mjini Beirut na Mogadishu.Hii yote imewafunza wamarekani kutumia nguvu kupita kiasi,lakini si rahisi hivyo kutatua matatizo na natumai wamarekani wametambua hayo.“

Alisema jamadari Cross.

Cross alikuwa afisa wa hadhi ya juu kabisa wa kijeshi wa Uingereza aliehusika na kutunga mkakati uliofuatia vita nchini Iraq. Jamadari Cross aliliambia gazeti la Sunday Mirror kwamba alimuarifu wasi wasi wake huo waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani,Donald Rumpsfeld,lakini hakumsikiza.