1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yanawa mikono?.

Halima Nyanza(zpr)8 Desemba 2010

Marekani imeachana na juhudi zake za kumshawishi Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuongeza tena muda wa siku 90, kuzuia ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi.

https://p.dw.com/p/QSrC
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Picha: AP

Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la New York Times toleo la leo, ambalo limewanukuu maafisa wawili waandamizi serikalini.

Serikali ya Rais Barack Obama wa Marekani, ilikuwa na matumaini kwamba siku 90 za kuzuia kwa muda ujenzi huo, zingetoa muda zaidi kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israel na Wapalestina kuweza kupata  mafanikio.

Benjamin Netanyahu bei einem Treffen mit Barack Obama
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Barack Obama.Picha: AP

Hata hivyo Waziri mkuu wa Israel, hakuweza kulishawishi baraza lake la mawaziri kukubaliana na pendekezo la Marekani la kuipatia nchi hiyo ndege za vita ili kuzuia ujenzi huo.

Wapalestina walijiondoa katika mazungumzo baada ya kumalizika kwa muda wa kuzuia ujenzi katika ukingo wa magharibi Septemba 26, na kwamba Israel haikuongeza tena muda huo.