1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

marekani yapanga mikakati mipya ya jeshi lake kwa Afrika.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJN

Camp Lemonier, Djibouti, Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amewasili nchini Djibouti leo kuyatembelea majeshi ya Marekani yanayofanya kazi zake zenye lengo la kupata kuungwa mkono katika eneo hilo ambalo Marekani inaliona liko katika hatari ya kutumbukia mikononi mwa wanaharakati wa Kiislamu. Waziri huyo wa ulinzi atangalia operesheni dhidi ya ugaidi inayofanywa na wanajeshi wapatao 1,800 katika eneo la pembe ya Afrika , ili kufahamu jinsi wanavyoweza kutumbukizwa katika kikosi kipya cha Afrika cha jeshi la Marekani , chenye jukumu la shughuli zote za kijeshi za jeshi la Marekani katika eneo hilo. Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa inatarajia kikosi hicho kwa ajili ya Afrika kitajishughulisha zaidi kuliko vikosi vingine katika kazi za maendeleo na ya kiutu, ikiwa ni sehemu ya mahusiano ya kidiplomasia na umma ama matumizi madogo ya mabavu, ambapo Gates anaona ni muhimu kwa ajili ya kupata mafanikio katika mizozo hapo baadaye.