1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasaema matokeo ya Bali hayatoshi

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcHL

Washington:

Marekani imeyakosoa na kusema hayatoshi, matokeo ya mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.”Haitoshi kuyalazimisha peke yao mataifa ya viwanda yapunguze moshi wa sumu unaotoka viwandani.Mataifa muhimu yanayonyanukia yanabidi pia yachangie katika kuhifadhi hali ya hewa-amesema hayo msemaji wa Ikulu ya Marekani mjini Washington.Marekani inataka mataifa,mfano China,Brazil na India nayo pia yachangie katika juhudi za kupambana na kuzidi hali ya ujoto ulimwenguni.Hata hivyo serikali ya Marekani imeyataja maridhiano yaliyofikiwa Bali kua ni hatua muhimu mbele.Kansela Angela Markel wa Ujerumani ameyataja matokeo ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa kisiwani Bali kua ni “mafanikio makubwa.”Njia imepatikana sasa ya kuendelezwa mazungumzo kuweza kufikiwa lengo lililokusudiwa”-amesema kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel.